Monday, September 17, 2012

WASANII WATAKIWA KUTUMIA MAWASILIANO KWA MANUFAA


  Mkurugenzi wa Idara ya Utafidi, Mafunzo na Habari wa BASATA, Godfrey Lebejo, akizungumza katika Jukwaa la Sanaa jumatatu, kulia ni Katibu Mkuu wa CAJAtz, Hassan Bumbuli na kushoto ni Mtoa Mada, Benedict Chale kutoka TPDA.
Mwasilishaji wa mada ya Umuhimu wa Mawasiliano katika Sanaa, kutoka kituo cha TPDA, bwana Benedict Chale akizungumza  wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa.

Wasanii nchini wametakuwa kuboresha namna ya utumiaji wa njia mbalimbali za mawasiliano zinazopatikana hapa nchini na katika maeneo yao ili kujitangaza na kutafuta masoko ya kazi zao.
 
Hayo yamesemwa katika Jukwaa la Sanaa, na Mkurugenzi wa Kituo cha Wakala wa Maendeleo ya Biashara  Tanzania (TPDA), Benedict Chale wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa Mawasiliano katika Sekta ya Sanaa hapa nchini.
 
“Tunatumia vipi fursa kubwa ya mawasiliano iliyopo katika shughuli zetu za sanaa? Hili ni swali la msingi, ukweli ni kwamba kumekuwa na tatizo la jinsi ya kutumia fursa hizi za mawasiliano kiufanisi. Ni muhimu sana wasanii wakaboresha namna ya kutumia haya mawasilinao katika kufanikisha kazi, kujenga mtandao, kutafuta na kuimarisha masoko na mambo mengine ya muhimu,” alisema Chale.
 
Alisema licha kuwepo kwa unafuu mkubwa katika mawasiliano kuanzia katika simu hadi intanet bado wasanii wanashindwa kutambua mbinu hasa za kutumia nafasi hiyo kufanya mawasilino yatakayowaletea manufaa zaidi na kuwataka kubadilika.
 
“Nawaomba wasanii washiriki pia katika maonyesho ya kazi mbalimbali za wasanii wengine na wajasiliamali,  kufanya hivyo ni kuongeza wigo wa mawasiliano, wengi wakiona ni maonyesho na picha basi mwigizaji haendi, basi isiwe hivyo, tenga muda nenda kunafaida fulani utaipata tu,” alisema.
 
Akihitimisha mjadala wa Jukwaa la Sanaa, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa BASATA Godfrey Lebejo, alitoa wito kwa wasanii kutumia pia fursa ya uwepo wa mawasiliano rahisi kujitafutia maarifa  na ujuzi kutoka katika mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na kujenga urafiki na wasanii katika maeneo mbalimbali Duniani.

No comments:

Post a Comment