Wednesday, October 24, 2012

BLOGU YA BIN ZUBEIRY YASHINDA TUZO YA COPA COCA COLA 2012



Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma ya Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa (kulia), akimkabidhi Mahmoud Zubeiry aka BIN ZUBEIRY wa bongostaz.blogspot.com (kushoto) mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 2, baada ya kushinda tuzo ya Mwandishi bora wa blogs wa mashindano ya Copa Coca Cola. Wengine katikati ni Meneja wa Sprite, Warda Kimaro na Katibu wa TASWA, Amir Mhando.

 KAMPUNI ya Coca Cola Kwanza, leo imewapa tuzo Waandishi watano wa Habari nchini, baada ya kuibuka vinara katika tuzo za Waandishi Bora wa mashindano ya soka ya vijana kwa umri chini ya miaka 17, Copa Coca Cola yaliyofanyika Julai mwaka huu.
Upande wa Blogs, bongostaz.blogspot.com ya BIN ZUBEIRY imeibuka kinara na kuzawadiwa Sh, Milioni 2 sawa na washindi wengine, upande wa Televisheni, Jimmy Tara wa ITV, Radio, Amry Masare wa Radio One, Magazeti, Japhet Kazenga wa Daily News na Mpiga Picha, Mohamed Mambo wa Habari Leo.
Tuzo hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa Coca Cola Kwanza, Evans Mlelwa, makao makuu wa kampuni hiyo ya vinywaji baridi, Mikocheni, Dar es Salaam.
Mchakato wa kutafuta washindi uliendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambacho leo kiliwakilishwa  na Katibu wake, Amir Mhando.

HONGERA SANA SWAHIBA

No comments:

Post a Comment