Saturday, October 27, 2012

MAMA ASHA BILAL ASHEREHESHA USIKU WA TAMASHA LA MWANAMKE MJASILIAMALI TANZANIA


 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wanawake Wajasiliamali, wakati wa Tamasha la Usiku wa Mwanamke Mjasiliamali lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, jana usiku.
 Mama Asha akisalimiana na baadhi ya wanawake wajasiliamali wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Serena Hoteli jana usiku.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, (wa  nne kulia) Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wa tatu kulia), wakijumuika na baadhi ya Kinamama kuserebuka kwa pamoja wakati wa Tamasha la Usiku wa Mwanamke Mjasiliamali Tanzania, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, jana usiku.
 Baadhi ya wanawake Wajasilimali, waliohudhuria Tamasha hilo.
 Baadhi ya Maofisa waalikwa kotoka Ofisi ya Makamu wa Rais, waliohudhuria Tamasha hilo, jana usiku.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, (wa  tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake Wajasiliamali  wakati wa Tamasha la Usiku wa Mwanamke Mjasiliamali Tanzania, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, jana.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Terezya Huvisa (kushoto) wakiwa Meza Kuu pamoja na baadhi ya viongozi wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la usiku wa Mwanamke Mjasiliamali,  lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, jana.
 Baadhi ya Kinamama Wajasiliamali waliohudhuria Tamasha hilo, wakiserebuka kwa raha zao.
 Hawa nao wakipozi kwa picha...

No comments:

Post a Comment