Friday, October 12, 2012

THT YAANZISHA DARASA LA MUZIKI NA VOCAL KILA MWEZI


 Mwalimu Kibaso ambaye anafundisha masuala ya Sauti (Vocal) akiwapa mazoezi ya viungo vijana waliojiunga katika darasa la muziki linaloendeshwa na Tanzania House of Talent (THT) kila mwezi jijini Dar es Salaam. Darasa hili limekuja kutokana na maombi ya vijana wengi wanaopenda kujifunza muziki.
 Vijana wakiwa katika mazoezi ya viungo ambayo yanasaidia kuwafanya wawe na pumzi ya kuimba.
 Kila mmoja akijiachia kwa bidii kufanya mazoezi.
 Akinadada nao hawapo mstari wa nyuma katika kufanya mazoezi.
 Mazoezi ya viungo yanaendelea, ambapo vijana wengi walipendezwa nayp japo ilikuwa ni mara ya kwanza walionekana kuchoka.
Baada ya kumaliza mazoezi ya viungo vijana walirudi darasani kwa ajili ya kupata masomo zaidi, mwalimu Kibaso akiwaimbisha wanafunzi wake.
 Mwalimu Magawa ambaye yeye ni mtaalamu wa Vyombo (Instruments), akimsikiliza mwanafunzi ambaye alipata nafasi  ya kujielezea maisha yake.
 Wanafunzi wakimsikiliza mwalimu Magawa ambaye aliwafundisha mabo mengi likiwemo suala la kujua aina ya muziki.

2 comments:

  1. Mimi nashida ya kuingia kwenye t h t kufanya mziki naomba mnisaidie niingie please, naweza luandika mistari ya rnb, hip hop ya marekani, nihisi nikiingia nitainyanyua T H T

    ReplyDelete
  2. Namba yangu ya SIMU +255763531689

    ReplyDelete