Monday, October 22, 2012

TIGO YAZINDUA MAJUKWAA YA UJASILIAMALI NCHINI

Tigo ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 Tanzania bara na Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshaji wa huduma zake za simu nchini Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano mpaka katika kutoa huduma za internet zenye kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu kupitia Tigo Pesa.

Huduma ziliboreshwa toka mlangoni.
Mwezeshaji wa Jukwaa kutoka Tigo Makao makuu  Hubert Luis  akifungua Jukwaa hilo ndani ya Hoteli ya Gold Crest Mwanza kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutirrez. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leoimezindua majukwaa kwa ajili ya wajasiliamali wapya nchi nzima kama sehemu ya wajibu wake katika kusaidia na kukuza wajasiliamali wadogowadogo na wakati nchini.

Lengo la majukwaa hayo ni kuwaleta pamoja wajasiliamali na mashirika ya kibiashara kutoka sekta mbalimbali ili kupanua mitandao yao na kunufaika na suluhu mpya za mawasiliano kwa biashara. Biashara ndogo na za kati zitanufaika na warsha, mafunzo na mazungumzo ya mada zinazohusu masoko, menejimenti, fedha na uzalishaji.

Ridhiwani Kassimu mtaalamu wa biashara ndogondogo na kati kutoka benki ya NBC akitoa somo. Pamoja na kufafanuwa kuhusu vifurushi maalum vya kiteknolojia vya mawasiliano, bwana Ridhiwani Kassimu mtaalamu wa biashara ndogondogo na kati alitoa somo kwa wajasiliamali na waendeshaji biashara kupitia mada ya "Jinsi ya kupata mitaji kwa biashara yako"

No comments:

Post a Comment