Monday, October 29, 2012

WAKALI 12 WA 'THE MIC KING' WAPATIKANA KUTOKA KINONDONI


Washiriki wa shindano la The Mic King, waliofuzu kuingia 12 bora kutoka Kinondoni wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Kundi la Wakali Dancers likiwajibika stejini.
USIKU wa kuamkia leo kulifanyika mchujo mkali wa kuwasaka wakali 12 kutoka Kinondoni wa shindano la The Mic King, ndani ya Ukumbi wa burudani wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam. Baada ya kumenyana vikali kwenye steji hiyo huku wakifuatiliwa kwa makini na majaji wanaoujua muziki vilivyo John Dilinga (Dj JD), na Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, ambao walifanya upembuzi makini na kuwapata wakali hao ambao ni Martin Gasper, Jafaar Kassim, Lusajo Kapngala, Peter Lugaman, Emmanuel Clemence, Ally Zuberi, Abdi Salim, Omary Xavery, Modestus Luiza, Athuman Ayoub, Dickson Siwalaza na Hudu Juma.
Shindano hilo pia lilisindikizwa na burudani za muziki kutoka kundi la Wakali Dancers na bendi ya Taarab ya Mashauzi Classic.
Majaji wa mchakato huo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (kushoto) na John Dilinga (Dj JD) wakiwa kazini.
Isha Mashauzi akiwarusha roho mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Dar Live.
Mpiga kinanda maarufu Bongo, Thabit Abdul akitumbuiza jukwaani.

No comments:

Post a Comment