Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linapenda kuwataarifu kuwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura
ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa
watakaoshughulikia masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa
Wanawake zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea. Uteuzi huo umefanywa na Rais
wa CAF, Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo za
Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika
Novemba 11, 2012. Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia
habari kwenye fainali hizo. Wengine ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF, Mahmoud
Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola. Wambura atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye
Kamati ya Maandalizi ya fainali hizo, kitu ambacho TFF inajivunia kutoa
mwakilishi kwenye moja ya mashindanoi makubwa ya mpira wa miguu Tanzania. Rais
wa TFF, Leodegar Tenga ameelezea uteuzi huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri
ambayo Wambura amekuwa akiifanya tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka 2011.
“Taarifa zake mbalimbali zimeifanya Tanzania iwe inang’ara CAF na hata FIFA kwa
kuwa kwa sasa wanajua kila kinachoendelea kwenye soka la Tanzania,” alisema Rais
Tenga na kumtakia Wambura kila la kheri kwenye kazi hiyo atakayoifanya kwa
takriban siku 14. Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, akizungumza kwa niaba ya
Sekretarieti, amemtakia Wambura kazi njema na kwamba awe kioo cha mabadiliko
makubwa yanayoendelea kwenye soka la Tanzania. Wambura alijiunga na TFF Januari,
2011 akiwa mmoja wa waajiriwa watatu wapya kwenye Shirikisho baada ya
wsatendajiu wengine wawili kumaliza muda wao wa mikataba. Wambura ni mwandishi
wa habari mwandamizi ambaye ameshafanya kazi kwenye vyombo mbalimbali kuanzia
kazi ya uandishi hadi Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo ambalo alikuwa
akifanya kazi kabla ya kujiunga na TFF Mahmoud Garga (CAF) Boniface Wambura
(Tanzania) Arlindo Macedo (Angola
No comments:
Post a Comment