Monday, October 15, 2012

WASHIRIKI WA MPANGO WA MAMA SHUJAA WA CHAKULA UNAODHAMINIWA NA NMB WATEMBELEA TAWI LA NMB MBEZI


Washiriki  wa mpango wa Mama Shujaa wa Chakula wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa benki ya NMB tawi la Mbezi walipo tembelea tawi hilo.
 
Washiriki wa mpango wa Mama  Shujaa wa Chakula wakipata mafunzo kutoka kwa Afisa wa Benki ya NMB tawi la  Mbezi.
 …………………………………………
Washiriki wa mpango wa Mama Shujaa wa chakula unaodhaminiwa na benki   ya NMB wametembelea tawi la NMB Mbezi na kuonyeshwa jinsi NMB inavyoendesha shughuli zake za kibenki katika matawi yake.
Washiriki hao waliongia katika kijiji cha Maisha Plus hivi karibuni, vilevile walipata fursa ya kupata elimu ya kifedha kupitia mpango wa NMB Financial Fitness.
NMB kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha iliwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.
 Vilevile, Washiriki hao walielimishwa kuhusu Mikopo Midogo na kati ya kibiashara pamoja na mikopo ya kilimo.
NMB inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.

No comments:

Post a Comment