Friday, October 19, 2012

ZOEZI LA KUKAMATA MAGARI YA SERIKALI YANAYOTUMIA NAMBA BINAFSI KUFANYIKA NCHI NZIMA



Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (waliokaa mbele wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu utaratibu wa usajili wa magari  ya Umma na kuwepo kwa zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba  za kiraia yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .

Baada ya hapo Operesheni kamata kamata magari, pikipiki, Bajaj na mitambo ya umma, itaanza na vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT, JW, DFP, CW, SM na SU.

Kwa mujibu wa Dk. Magufuli, hadi sasa serikali imeshasajili vyombo vya moto, 123,431 yakiwemo magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma.  Mkuu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed  Mpinga. PICHA/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO
 

Kaibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Hebert Mrango akifafanua jambo.

Dk. Magufuli akiteta jambo na Kamanda Mpinga..Kwa hisani Daily Mitikasi Blog

1 comment:

  1. I truly love your blog.. Great colors & theme. Did you
    make this amazing site yourself? Please reply back as I'm trying to create my own personal site and would like to know where you got this from or exactly what the theme is called. Many thanks!

    Here is my webpage - laser cellulite treatment

    ReplyDelete