Friday, November 30, 2012

AIRTEL Tanzania kumpongeza Balozi wake AY katika Bonge la Party ndani ya Nyumbani Lounge


Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya  Channel 'O'  aliyoipata Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa ushindi alioupa pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya video bora, Katikati ni AY  akifatiwa na DJ wake Athur Baraka.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kupata tuzo hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni  DJ wake Athur Baraka.
****************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya  “ AY “  na kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya kijulikanacho kama “   I don’t wanna be alone”

Akiongea na wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.

Naye Afisa uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii mbalimbali toka  Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa kusherehekea ushindi  huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu.

Tunapenda pia kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale nyumbani lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake

No comments:

Post a Comment