Tuesday, November 6, 2012

AIRTEL YATOA VITABU VYENYE THAMANI YA MILIONI 12/- KWA SHULE ZA SEKONDARI IRINGA


Meneja Uhusiano wa Airtel Kanda, Jackson Mbando (kulia) akimkabidhi kwa Diwani wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda, Tarafa ya Kiponzero, Ifunda Mkoani Iringa.  Wanaoshuhudia makabidhian o hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ni Katibu wa Mbunge wa Kalenga, Martin. Airtel ilitoa msaada huo wa vitabu kwa shule nne za jimbo la Kalenga mkoani Iringa. (Picha na Mpigapicha wetu).

Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda (kulia) akimkabidhi vitabu kwa Mkuu wa shule ya Sekondari Wasa iliyopo Ifunda Mkoani Iringa, David Mpalanzi. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki ni Katibu wa Mbunge wa Kalenga, Martin Simangwa (wapilki kulia) na Diwani wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda. Airtel ilitoa msaada huo wa vitabu kwa shule nne za jimbo la Kalenga mkoani Iringa. (Picha na Mpigapicha wetu).

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyandembela iliyopo Ifunda mkoani Iringa, wakisaidiwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mbando (kushoto) kushusha vitabu vya masomo ya Sayansi na Hisabati vilivyogawiwa katika Shule nne katika jimbo la Kalenga Mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. (Picha na Mpigapicha wetu).  
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

·Shule 4  za sekondari mkoani Iringa za faidi na msaada huo

Katika kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinainuka, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mpango wake wa Shule yetu imeendelea kutoa msaada wa vitabu kwa shule mbalimbali za sekondari ambapo mwisho mwa wiki hii Airtel ilitoa vitabu kwa shule za sekondari Kiponzelo, Wasa, Mgawa and Lyandembela zilizoko mkoani Iring.

Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Lyandembela Tarafa ya Kiponzero, Ifunda Mkoani Iringa, Diwani wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda,  alisema “Tunashukuru Airtel kwa kutoa haki sawa kwa shule zote nchini kwa kuchangua shule kupitia droo ambayo imeweza kuwafikia wanafunzi wa shule za Iringa hadi vijijini. Tumefurahi sana kupata vitabu mbalimbali kwani shule ya sekondari za hapa Ifunda zina  changamoto ya upungufu wa vitabu hasa vya sayansi na kulifanya somo hilo kuwa na wanafunzi wa chache, lakini hivi sasa kutokana na msaada wa vitabu vilivyo tolewa vitaongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu”.

Nachukua fulsa hii kuwaasa wanafunzi wavitumie vitabu hivi vizuri na kujiunga na masomo ya sayansi, tunaamini vitabu hivi vitaleta ufanisi pamoja na kuwa na changamoto ya walimu naahidi kuwashirikisha wizara ya elimu ili kuongeza idadi ya walimu wa sayansi na kuongeza ufaulu zaidi” aliongeza Bi Mwenda

Naye Mwalimu mkuu wa sekondari ya Wasa David Mpalanzi Iliyoko Wilaya Mfindi Mkoa wa Iringa akiongea kwa niaba ya wakuu wa sekondari wa shule za Mgama, Lyandembela and Kiponzelo alitoa shukurani kwa Airtel na kusema msaada huo wa vitabu utaweza kuwa saidia wanafunzi kuwa na uweza wa kujisomea zaidi na kuwawezesha kufaulu hadi kwenda chuo kikuu,kwani hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa katika shule zetu ambapo uwiano ulikuwa kitabu kimoja wanafunzi 15 hadi 20. Lakini msaada huu utapunguza zaidi, kwa kweli huu ni msaada mkubwa katika kuboresha taaluma na kuinua ufaulu hivyo tunaomba program hii ya shule yetu iendelee ili kuwafikiwa watu wengi zaidi

Tunaomba Airtel muongeze wigo wa kutoa misaada mbalimbali ya kuboresha elimu na mazingira kwa ujumla ikiwemo , kutoa komputa, kusaidia upatikanaji wa maji, na mengine mengi.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi Kaka Mkuu wa shule ya Lyandembela sekondari Taifa Malata ametoa shukurani kwa niaba ya wenzao huku akibainisha wanafunzi wengi walikuwa wakifeli katika masomo mbali mbali kutokana na ukosefu wa vitabu ,wanafunzi hao wameomba uongozi wa Airtel kuwafikirili kutatua changamoto zingine kama ukosefu wa maji, pamoja na kuwajengea maktaba ya kuwatosheleza ili kujisomea kwa nafasi zaidi

Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja mauzo wa Airtel Beda Kinunda amewataka wanafunzi wa sekondari zote mkoani Iringa kuongeza uwezo wa kujisomea ili Airtel ione ufaulu wa wanafunzi unaongezeka kupitia msaada unatolewa na Airtel,  pia natoa wito vitabu hivi vitunzwe ili viweze kuwafaidisha wanafunzi wengi kwa kuwa Airtel imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu ili iwe chachu kukuza Elimu.

Airtel imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu ili kuendeleza Elimu Inchini Tanzania Umeanzisha Mpango huo na kuweza kushindanisha shule mbalimbali zaidi shule 3000 na shule zinazo shinda hupewa vitabu katika bahati na sibu hiyo. shule NNE za mkoa wa Iringa zilibahatika kushinda.

No comments:

Post a Comment