Thursday, November 29, 2012

BENDI YA MASHUJAA NA JB MPIANA KUZINDUA 'RISASI KIDOLE' KESHO IJUMAA


 Wanamuziki wa bendi ya Mashujaa, wakiongozwa na Chalz Baba (katikati) wakijifua wakati wa mazoezi yao ya maandalizi ya uzinduzi wa Albam yao ya pili inayokwenda kwa jina la Risasi Kidole, uzinduzi unaotarajia kufanyika kesho katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, huku ukisindikizwa na mwanamuziki mahiri kutoka Congo, JB Mpiana.
Kiongozi wa bendi hiyo, Chalz Baba, akiongoza mashambulizi wakati wa mazoezi hayo ya maandalizi leo.
************************
BENDI ya Mashujaa kesho siku ya Ijumaa itazindua albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la Risasi Kidole pamoja na bendi maarufu ya Congo, Wenge BCBG iliyochini ya mwanamuziki JB Mpiana kwenye  viwanja vya Leaders club, Kinondoni.
Uzinduzi huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa meneja wa bendi ya Mashujaa, Martin Sospeter. Sospeter alisema kuwa wamejiandaa vilivyo katika uzinduzi huo na lengo lao kubwa ni kuweka historia katika muziki wa Tanzania.
Alisema kuwa wamekaa kambini muda wa siki mbili na wameandaa vitu vingi vipya kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi nchini. Alisema kuwa kuna rap ya Ua Mbu na Dume la Simba kutoka kwa marapa wao, Saulo Ferguson na Sauti Radi.
Alifafanua kuwa wanamuziki wake wameadhimia ‘kufunika’ katika uzinduzi huo kwani anahistoria nzuri katika muziki wa Tanzania na kufanya kazi katika bendi nyingi.
“Tunawaomba watanzania waje waone nini tunakifanya mbele ya gwiji la muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana, najua wao wamepania, lakini sisi tumepania vilivyo kusafisha nyoyo za mashabiki ambazo kwa sku nyingi hawajapata burudisha la mioyo zao,” alisema.
Kiongozi wa bendi hiyo, Charlz Baba alisema kuwa wamepania kutoa somo kwa wanamuziki wa dansi hapa nchini ambao wamekuwa wakisubiri waone watafanya nini. Alisema kuwa wameandaa nyimbo nyingi nzuri  na wamepatia kutawala soko la muziki hapa nchini.
“Njooni muone nini tunafanya katika muziki wa dansi, kambi yetu imekuwa nzuri na mafanikio makubwa, naomba mashabiki waje kutuunga mkono nasi tutawaunga mkono kwa kutoa burudani safi,”alisema Chalz.
Albamu ya Risasi Kidole ina jumla ya nyimbo sita. Nyimbo hizo ni Umeninyima, Tikisika, Hukumu ya Mnafiki, Ungenieleza, Kwa Mkweo na wimbo uliobebab jina la albamu hiyo, Risasi Kidole

No comments:

Post a Comment