Thursday, November 29, 2012

BODI YA UTALII (TTB) YAPEWA CHETI KWA MCHANGO WAKE DHIDI YA MAPAMBANO YA MALARIA KATIKA UZINDUZI WA MPANGO WA KUTOKOMEZA MALARIA UNAOITWA “MALARIA SAFE”



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuitambua kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya Malaria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na ugonjwa huo inayoitwa (Malaria Safe Companys) uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jijini dar es salaam usiku huu ambapo Wizara ya afya inashirikiana na pamoja na taasisi za kimataifa na Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi akimpongeza Bw. Geofrey Meena baada ya kupokea cheti hicho kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Mzee CHrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama ya mkoani Rukwa kwa mchango wake katika kupambana na Malaria nchini.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadau makampuni na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini mara baada ya uzinduzi huo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya kupambana na Malaria inayoitwa "Malaria Safe Companys" , kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Raymond Mushi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Rais Washirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Bw. Leodger Tenga wakati alipowasili katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria, kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi.
Wadau waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria kutoka kulia ni Mkurugenzi wa michezo katika Wizara ya Habari, Vijana , Michezo na Utamaduni Bw. Leonald Thadeo, Assah Mwmbene Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Mbunge wa Jimbo la Temeke Mh. Abbas Mtemvu na Mbunge na Waziri wa zamani Mh. Chrisant Mzindakaya.
Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo katika Hyatt Regency Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Sahara Media Bw. Samwel Nyala kushoto akiwa na wadau wengine katika uzinduzi huoHyatt Regency Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiandika kitu huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Hussein Mwinyi akipiga makofi katika uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Mzee Salim Mohamed Abeid Bakhressa akitoa ushuhuda kuhusu malaria ilivytokomezwa katika viwanda vyao.
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Bw, Leodger Tenga akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jinsi sekta ya michezo ilivyosaidia kutokomeza malaria nchini.
 
Mwimbaji nguli wa muziki wa Taarab Khadija Kopa pamoja na kundi lake wakitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment