Sunday, November 4, 2012

BRIGITER ALFRED ANYAKUA TAJI LA REDDS MISS TANZANIA 2012


Mshindi wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brighter Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili, Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo. Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene anatoka Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa huku Edda ni Miss Kigamboni na Kanda ya Temeke.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatu5 bora ya Redds Miss Tanzania 2012, kutoka kushoto ni Brigitte Alfred, Eugen Fabian, Happyness Daniel, Edda Sylvester na Magdalene Roy wakipozi kwa picha.

Washiriki wakicheza show ya ufunguzi wakati wa kuanza kwa shindano hilo.
Wageni mbalimbali na wadau wa tasnia ya Urembo nchini Tanzania wakifuatilia shindano hilo kwa umakini ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la Ngoma za Asili la Wanne Stars likitoa burudani.
Balozi wa Tanga Beach Resort, Happyness Rweyemamu akijinadi jukwaani na vazi lake la ubunifu.
Mshiriki Flavian Maeda kutoka Kitongoji cha Kurasini na Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam akipozi jukwaani na vazi la ubunifu.
Fina Recatus akipita jukwaani na vazi la ubunifu. Fina ni Balozi wa Tanga Beach Resort 2012.
Naomi Jones nae akipita jukwaani na vazi la ubunifu
Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Kudra Lupato akikatiza jukwaani.

No comments:

Post a Comment