Monday, November 12, 2012

Ki-COLLEGE ZAIDI NA NMB YAWATUNZA WANAFUNZI 66


 Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro akionesha zawadi ya taa ya kutumia mionzi ya jua 
 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah akibonyeza kitufe cha kompyuta kuwatafuta washindi wa promosheni hiyo.
 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah (wa pili kulia) akiangalia namna washindi wa promosheni ya Ki-College Zaidi na NMB wanavyopatikana wakati wa droo ya kwanza iliyochezeshwa Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdulhussein. Kushoto ni Meneja wa Amana, Boma Raballa na Meneja Masoko, Shilla Senkoro

Na Salum Mkandemba
BENKI ya NMB, leo imewazawadia wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), Chacha Nyange Nchamcho na Kelvin Gabone, kila mmoja zawadi ya I Pad, katika promosheni ya Ki-COLLEGE Zaidi inayoendeshwa na benki hiyo.
Promosheni hiyo inayohusisha wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student, ilifanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo washindi wengine wawili walijishindia simu za mkononi aina ya Samsung Galaxy.
Jumla ya washindi 66 walipatikana katika droo hiyo, ambapo 60 kati yao walijishindia zawadi za taa maalum za kujisomea zinazotumia mionzi ya jua, fulana za NMB, jezi za Taifa Stars na ongezeko mara mbili la kaunti ‘Amana Maradufu.’
Akizungumza wakati wa promosheni ya kuwasaka na hatimaye kuwatangaza washindi hao, Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro, aliwataka wanafunzi kuendelea kufungua akaunti ya NMB Student au kuweka amana zao, ili kujishindia zawadi mbalimbali katika droo mbili zijazo.
Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya Ofisa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Abdulhussein, ni ya Oktoba, ambapo washindi wa mwezi huu watasakwa mwezi ujao, huku wateja wa droo ya mwisho ya Desemba, watatafutwa Januari mwakani
Senkoro aliongeza kuwa, nia ya promosheni hiyo ni kurudisha sehemu ya faida yao kwa wateja, hususani wanafunzi kupitia akaunti maalum iliyoanzishwa mwaka 2007, kutokana na ongezeko la vyuo vya elimu ya juu nchini vilivyoongeza idadi ya wateja.
Alisema kuwa, hadi sasa akaunti ya NMB Student ina zaidi ya wanafunzi 70,000, waliofungua katika matawi mbalimbali nchini, huku akiwataka wengine kuendelea kujitokeza ili kujishindia zawadi zitakazotoa msukumo wa maendeleo yao kimasomo.

No comments:

Post a Comment