Monday, November 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU MKOANI KATAVI


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa, wakati alipofika katika Kijiji cha Ilembo Mkoa wa Katavi, Nov 24, kwa ajili ya kuzindua rasmi Ujenzi wa Nyumba za gharama nafuu, zinazojengwa na Shirika hilo, ambapo jumla ya nyumba 250, zinatarajia kujengwa katika eneo hilo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,  Nehemiah Kyando Mchechu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye (wa pili kulia) wakikagua sehemu ya ujenzi wa nyumba hizo bada ya uzinduzi wa mpango wa Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC, katika kijiji cha Ilembo Mkoani Katavi Nov 24, 2012.

No comments:

Post a Comment