Monday, November 19, 2012

Mh. Lowassa aongoza Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Babati Mkoani Manyara


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa hilo Usharika wa Babati,Mkoani Manyara leo.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni (wa tatu kulia) akizungumza wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara leo.Wengine pichani toka Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Harambee hiyo),Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri na Kulia ni Diwani wa kata ya Endamilay (CCM) Gesso Bajuta.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpongeza Mbunge wa Viti maalum Mkoani Manyara (Chadema),Mh. Pauline Gekul mara baada ya kuchangia kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara leo.Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendelea kupokea michango mbali mbali kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara leo. 
Baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wakiwa kwenye Harambee hiyo ya Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara leo.

Na mwandishi wetu

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh Edward Lowassa amesema wakati umefika sasa hapa nchini elimu ya sekondari iwe ni elimu inayotolewa bure na kumwondolea mwananchi mzigo .

Lowassa amesema hayo leo mjini Babati wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati.

Alisema kwa sasa kila kata hapa nchini ina shule ya sekondari na huo ulikuwa mpango wake akiwa Waziri Mkuu na alisimamia kikamilifu suala hilo na kufanikiwa kwa asilimia mia moja.Shule hizo za kata ni maarufu kama shule za Lowassa.

Hata hivyo kiwango kinachotolewa na shule hizo ni cha chini sana.

Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli alisema sasa wakati umefika kwa kila mtanzania kulizungumzia suala hilo bila ya woga hususani wadau wa elimu na kuongeza kuwa.

''Ni lazima tukubali na tujadili suala hilo kwa manufaa ya nchi kwa kila mtanzania kukubali ushauri huo wa elimu ya sekondari kuwa ya bure''alisisitiza na kuongeza kuwa kuwa ni vyema baada ya kulijadili suala hilo la elimu ya bure ya sekondari tena elimu iliyo bora liwemo kwenye ajenda za Chama cha Mapinduzi (CCM) za uchaguzi mkuu wa 2015.

Lowassa alisema kuwa hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alitoa wito kwa shule za sekondari kujenga maabara kwa wingi,hivyo kwa hiyo amesema ni suala linalopaswa kuungwa mkono na kila mtanzania na pia elimu ya bure katika sekondari nayo inapswa kuungwa mkono.

‘’Nasema sasa wakati umefika elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya msingi kwa watoto kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ‘’alisema.

Lowassa aliwaasa pia wadau mbalimbali hapa nchini kuwa mstari wa mbele kuchangia elimu ili nchi hapo baadae iwe na vijana wenye elimu ya kutosha na ya hali ya juu.

No comments:

Post a Comment