Monday, November 12, 2012

MIYAYUSHO NASSIBU KUZIPIGA 9 DESEMBA


Fransic Miyayusho
BONDIA Fransic Miyayusho yupo katika mazoezi ya mwisho kujiandaa na mpambano wake na bondia Nassibu Ramadhani litakalofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba tarehe 9 desemba mpambano utakaoamua nani bondia bora wa mwaka huu kutokana na Nassibu Ramadhani kuwa bondia bora wa mwaka kwa mwaka 2012

Miyayusho ambaye anapiga kuwa Nassibu kuwa bora kuliko yeye ndio mana ukandaliwa mpambano baina yao kutokana na hilo mpambano huo unaotarajiwa kuvuta hisia za watu wengi hususani kutoka maeneo ya Kinondoni anapotokea bondia Miyayusho na Mabibo pamoja na maeneo ya Manzese na ubungo ambapo anatokea bondia Nassibu

Katika mchezo huo kutakuwa na mapambanmo kadhaa ya utangulizi likiwemo la bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Said Mundi wa Tanga mpambano wa mabondia wanao tamba kwa sasa kwani wao ndio wapo katika kiwango bora ndio mana wamepambanishwa kwa siku hiyo

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali

No comments:

Post a Comment