Friday, November 30, 2012

MKUTANO MKUU WA NAMANGA SPORTS CLUB KUFANYIKA DESEMBA 09 NDEGE BEACH


Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu, kilichofanyika Leecar's Pub Namanga jijini Dar es Salaam. PICHA/JOHN BADI
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

- KONYAGI yaupiga 'Jeki'

Na John Badi
 
Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu ya Namanga Sports unatarajiwa kufanyika Desemba 09, mwaka huu katika Ukumbi wa Ndege Beach uliopo katika eneo la Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi, Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, Bw. David Mwaka alisema tayari makampuni kadhaa yameshajitokeza kudhamini mkutano huo.

Bw. Mwaka aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Tanzania Distilleries Ltd watengenezaji wa kinywaji maarufu cha Konyagi, Mike Commercial, Esoshi General Trading Co. Ltd na Mele DJ Co. Ltd ya Dodoma.

"Tunawashukuru sana wadhamini ambao tayari wamekwisha onyesha moyo wa kutusaidia, lakini pia tunawaomba wadhamini wengine wajitokeze zaidi ili tuweze kufanikisha mkutano wetu", alisema Bw. Mwaka.

Aidha Bw. Mwaka alitoa wito kwa wanachama wa klabu hiyo ambao bado hawajatoa michango yao ya 20,000/- kuiwasilisha mara moja kwa watu waliopewa majukumu ya kukusanya ambao ni John Gako, Bebee Mangi na Chale JJ.

No comments:

Post a Comment