Monday, November 26, 2012

My Everything ya Alikiba yasikika redioni



Na Elizabeth John
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini Ali Kiba baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘My everything’.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Alikiba amesema alikuwa kimya kwa muda mrefu sasa amejipanga na ameamua hivyo mashabiki wakae tayari kupokea burudani kutoka kwake.

“Nilikuwa kimya kwa muda mrefu sasa nimejipanga na nimeamua kutoa burudani kwa mashabiki wangu hivyo watarajie vitu vizuri mfurulizo kutoka kwangu,” amesema Alikiba.

Amesema sasa anatarajia kutoa vitu mfululizo kwaajili ya kuwapa burudani mashabiki wake na kudai kuwa baada ya wiki mbili mbele atakuwa ameanza kusambaza video ya kibao hicho.

“Kkwasasa ukichelewesha kutoa video wimbo unachuja haraka hivyo [sipo tayari kuaribu kazi yangu nimejipanga na nimeamua ntaakikisha video inatoka mapema kabla ya kibao hicho kuchuja,” amesema Alikiba.

No comments:

Post a Comment