Thursday, November 22, 2012

Nicolas Cage apunguza deni la kodi



 NEW YORK, Marekani

MWIGIZAJI wa filamu nchini hapa, Nicolas Cage amepunguza deni la kodi analodaiwa kwa kulipa kiasi cha dola 600,000.

Baada ya kulipa kiasi hicho cha fedha hivi sasa mwigizaji huyo atakuwa akidaiwa kiasi cha dola milioni 6.

Mwigizaji huyo amekuwa akidaiwa kiasi hicho cha fedha kutokana na kuwa bingwa wa kukwepa ulipaji wa kodi.

Cage alijimwagia sifa kwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa kusema kwamba amepunguza deni ambalo limekuwa likisumbua akili zake.

No comments:

Post a Comment