Friday, November 23, 2012

SAFARI LAGER KUZINDUA MSIMU WA PILI WA PROGRAMU YAWAJASIRIAMALI YA “SAFARI LAGER WEZESHWA” JIJINI MBEYA LEO.


Balozi wa Safari Lager Wezesha, Janeth Karabu(kushoto) akiwaelimisha wakazi wa Iringa Mjini kuhusu Safari Lager Wezeshwa awamu ya pili Mkoani hapo mwishoni mwa wiki.

Balozi wa Saafari Lager Wezesha, Sarafina Msawe(katikati) akiwaelimisha wakazi wa Iringamjini kuhusu programu ya Safari Lager Wezeshwa  awamu ya pili iliyozinduliwa mwinshoni mwa wiki Mkoani hapo.

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager             leo inatarajia kuzindua rasmi msimu wa pili wa programu ya kuwaelimisha wajasiriamali wa jijini Mbeya juu ya “Safari Lager Wezeshwa”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema timu ya Mabalozi 15 wa ya kuelimija jamii imeshawasili jijini Mbeya tayari kuanza kutoa elimu kwa jamii ya wakazi wa Mbeya hasa wafanyabiashara ndogo ndogo na wa kati juu ya programu ya Safari Wezeshwa.
Alisema Shelukindo, timu hiyo ilianzia Mkoani Kilimanjaro,Arusha,Mwanza,Shinyanga,Morogoro,Iringa na Tanga ikielimisha jamii ya Watanzania juu ya programu hiyo na sasa leo ni jijini Mbeya ambapo watafanyakazi katika viwanja vya Malimbali vya jijini Mbeya kwa siku mbili wakielimisha jamii juu ya Safari Lager Wezesha  na baada ya hapo watahamia Mkoani Lindi na Mtwara.
Programu  hii ilipata mafanikio makubwa, mwaka jana iliwawezesha wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Bwana Shelukindo alisema, “Safari Lager kwa mara ya pili  inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaoingia na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali
kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.
Shelukindo alimaliza kwa kuwapa changamoto wajasiriamali kujitahidi zaidi sio tu kwa ajili ya kujishindia ruzuku za programu ya“Safari Lager Wezeshwa” lakini kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. Aliwasihi wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla kutega sikio kwa taarifa zaidi juu ya usajili na kutembelea website ya www.wezeshwa.co.tz.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.

No comments:

Post a Comment