Thursday, November 22, 2012

Tamasha la Jinsia Morogoro



 Mgeni rasm na Mkuu wa Chuo cha Jinsia Dk. Diana Mwiru wakifuatilia tamasha la Jinsia  ngazi ya wilaya linaloendelea katika viwanja vya MOSEKA Mkamabarani Morogoro Vijijini, kuanzia 21-23 Novemba 2012. washiriki zaidi ya  400 wamejitokeza kwa siku ya kwanza huku tukitarajia ongezeko kubwa la wan anchi siku ya leo kutokana na msisimko mkubwa wa mada na wananchi wengi kutaka kuzungumzia kero zao, kwa siku ya jana.  Jana  kilio kikubwa kilikuwa ni Migogoro ya ardhi na uongozi mbovu.

 Wanaanchi wa Mkambarani
 Wananchi wa Morogoro walioshiriki tamasha wakiendelea kusikiliza watoa mada
Ni burudani kila mara kuondoa uchovo

WABUNIFU 23 KUTOKA TANZANIA KUONYESHA UBUNIFU WAO



Meneja wa Swahili Fashion Week, Washington Benbella akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Swahili Fashion Week 2012. Kutoka kushoto ni Hassan Mrope, Meneja Mahusiano wa Swahili Fashion Week, Happy Shame Meneja Masoko EATV..JPG



DAR ES SALAAM, Tanzania
Onyesho kubwa la mitindo la Afrika Mashariki na kati linarajiwa kufanyika siku tatu mfululizo katika Hoteli ya Golden Tulip kuanzia tarehe 6, 7 na 8 Desemba, 2012 ikiwa ni mara ya tano tangu kuanzishwa kwake.
Swahili Fashion Week 2012 kwa ujumla itakutanisha pamoja wadau 50 katika tasnia ya Mitindo kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na nyengine kuweza kuonyesha ubunifu wao na kutoa mustakabali wa mwenendo wa tasnia ya mitindo katika ukanda huu.
“Mwaka tumekuwa kwa kiasi kikubwa, wabunifu 23 kutoka Tanzania wataweza kuonyesha ubunifu wao na wengine waliobaki ni kutoka nje ya Tanzania, ambao wote wataonyesha ubunifu wao katika jukwaa moja ukiachilia wabunifu 16 walionyesha ubunifu wao katika maonyesha ya Swahili Fashion Week yaliyofanyika Nairobi, Kenya, Oktoba 6, 2012” Alisema Meneja wa Swahili Fashion Week, Washington Benbella
Katika kuongeza maonyesho ya mitindo, mwaka huu Swahili Fashion Week shopping Festival ambayo ilianza 2010 itakuwepo tena kwa mara nyengine ambapo itashirikisha zaidi ya waonyeshaji 30 katika sehemu moja ikiwa ni kwa ajili ya kuonyesha na kuuza bidhaa za ubunifu hivyo kuifanya kuwa msimu mkubwa manunuzi ya kazi za ubunifu wa mitindo hapa Tanzania.
Kama ilivyo ada, Swahili Fashion Week inatoa nafasi kwa kuendeleza vipaji, ambapo tarehe 24 Novemba, 2012 kutakuwa na mchujo wa wazi kwa wanamitindo wapya na wanaochipukia kwa jinsia zote, na mnamo tarehe 7 Desemba, 2012 kutakuwa na warsha kwa ajili ya wabunifu wote Tanzania chini wadhamini wakuu wa warsha hiyo USAID Compete ambayo itafanyika katika Hotel ya Golden Tulip” Aliongeza Benbella
Mashindano tofauti yamepangwa kufanyika wakati wa Swahili Fashion Week, ikiwemo Shindano la kumtafuta Mbunifu Bora anaechipukia na Mbunifu Bora wa kubuni Fulana. Sio tu inatoa changamoto na ari ya ushindani katika tasnia ya ubunifu nchini Tanzania, bali pia inaweka msingi imara kwa wabunifu wa baadae.
“Sherehe maalum za kufungua Swahili Fashion Week zinarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Novemba, 2012, Thai Village kuanzia saa 9 usiku. Sherehe hizo pia zitafuatiwa na kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa kushindania tuzo mbalimbali zilizowekwa katika vipengele 16, tuzo hizi ni za kwanza na ndio pekee katika ukanda huu. Tiketi za sherehe za uzinduzi wa Swahili Fashion Week 2012 zinapatikana sehemu zifuatazo, Thai Vilage, Mgahawa wa Epidor uliopo Masaki, na Tanzania Mitindo House” Alisema Meneja Uhusiano, Hassan Mrope
“Tukiwa na mipango yenye ndoto za kutangaza biashara ya mitindo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati, ninapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru washirika wetu pamoja na  wadhamini wetu ambao karibia ya wote wamekuwa wakitusaidia kutokea maonyesha yaliyopita mpaka sasa. Pia tuwashukuru sana watu wote wanaosaidia tasnia ya mitindo hapa Tanzania kwa si tu kuhudhuria matamasha na maonyesho kama haya bali pia kwa kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini kwani hii inatangaza kinachotengenezwa Africa “Made in Africa”. Alimalizia Benbella
Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania),  Perfect Machinery Ltd, Ndibstyles, PKF Tanzania and 361 Degrees

No comments:

Post a Comment