Monday, November 12, 2012

VODACOM WAMWAGA MIKOPO YA MILIONI 17 BUIGIRI DODOMA


 Mwanachama wa kikundi cha Upendo katika kijiji cha Buigiri mkoani Dodoma, Diria Yaledi Mtumwa (kushoto) akipokea fedha ikiwa ni mkopo unaotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom kwa kupitia mpango wake wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Mikopo ya jumla ya kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 17 ilitolewa kwa wanawake wa Buigiri na kukabidhiwa na Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon (kulia) huku Afisa wa Vodacom Ally Mbuyu (wa pili akishuhudia). Makabidhiano hayo ya awamu ya pili ya mikopo ya MWEI yalifanyika kijijini Buigiri mkoani Dodoma leo
 Mwanachama wa kikundi cha Upendo katika kijiji cha Buigiri mkoani Dodoma, Diria Yaledi Mtumwa (kushoto) akionesha fedha za mkopo alizokabidhiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom kwa kupitia Mpango wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Zaidi ya Sh. Milioni 17  zilitolewa kwa wanawake wa kijiji cha Buigiri, mkoani Dodoma leo

No comments:

Post a Comment