Thursday, November 8, 2012

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA UTALII YA WTM YANAYOFANYIKA JIJINI LONDON UINGEREZA


 
Waziri wa maliasili za Utalii Balozi Khamis Kagasheki akihojiwa na kituo cha Televisheni ya Taifa TBC mara baada ya kutembelea mabanda ya makampuni ya Tanzania yanayoshiriki katika maonyesho ya Utalii ya World Travel Market yanayoandaliwa na kufanyika katika eneo la Excell jijini London nchini Uingereza, yakishirikisha makampuni mbalimbali ya utalii kutoka pande zote za dunia, Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na makampuni zaidi ya 55 yakiwa chini ya Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB).
Waziri Balozi Kagasheki amesifushiriki wa makampuni ya Tanzania katika maonyesho hayo lakini amesisitiza kwamba makampuni hayo yaongeze juhudi za kutangaza utalii wa Tanzania mpaka kufikisha lengo la idadi ya watalii milioni moja kila mwaka, ameongeza kwamba kuna haja ya kuongeza vitanda zaidi nchini Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea katika mbuga zetu na kufanya utalii kuka zaidi, Maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi kesho.
Fullshangweblo iko jijini London nchini Uingereza ikikumuvuzishia matukio haya moja kwa moja kutoka katika maeneo ya Excell ambako ndiko maonyesho hayo yanafanyika.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
 
Waziri aliasili na Utalii wa Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Issa Ahmed Othman Mshauri wa Rais masuala ya Utalii Zanzibar wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM) jijini London leo nchini Uingereza
 
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Leila Ansel Mkuu wa mauzo na masoko kampuni ya Tanzania Zara Adventures wakati alipotembelea katika banda hilo leo kwenye maonyesho ya utalii ya WTM nchini Uingereza.
 
Yvone Baldwin Afisa mauzo wa kampuni ya ndege ya Precision Air akimkabidhi zawadi Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe mara baada ya kutembelea banda hilo leo akiongozana na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki.
 
Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Rashid Adam Meneja Masoko wa Tanzania Zara Adventures wakati alipotembelea maonyesho ya Utalii ya WTM katika banda la Tanzania leo jijini London, wa pili kutoka kushoto ni Mh. Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na katikati ni mama Balozi.
 
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Laura Meneja wa Maendeleo ya Biashara kampuni ya Laitolya Tours & Safari Ltd kushoto wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya WTM leo, kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akiwahudumia watu mbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania leo katika maonyesho ya Utalii ya WTM jijini London Uingereza
 
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa African Environments Richard Beatty na Janice Beatty katika maonyesho hayo.
 
Leila Ansel Mkuu wa mauzo na masoko kampuni ya Tanzania Zara Adventures akizungumza na mmoja wa wageni waliotembelea katika banda la kampuni hiyo katikati ni Rashid Adam Meneja Masoko wa Tanzania Zara Adventures.
 
Mh. Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza na mdau Juma Mabakila wakati akitembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho ya WTM
 
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwasikiliza wageni mbalimbali waliofika katika banda la Tanzania katika maonyesho hayo leo.
 
Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili Utalii wa pili kutoka kulia akizungumza na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania katika maonyesho ya Utalii ya WTM nchini Uingereza , kulia ni Mh. Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na katikati ni Mama Balozi.
 
Mmoja wa washiriki kutoka kampuni ya Africa Adventure akihojiwa na kituo cha televisheni cha TBC katika maonyesho ya Utalii ya WTM yanayofanyika jijini London nchini Uingereza.
 
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wakati alipotembelea maonesho hayo kushoto ni Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii nchini TTB.
 
Washiriki mbalimbali wakiwa katika banda la Tanzania wakipokea wageni mbalimbali wanaotemelea kwenye banda hilo kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu utalii wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment