Monday, December 10, 2012

CRDB YAZINDUA MIKOPO YA MAKAZI


 Meneja Mwandamizi Mahusiano ya Wateja wa CRDB, Silas Katemi (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana ya utaratibu mpya wa ukopeshaji pesa za ununuzi na ujenzi wa nyumba za makazi kwa wateja wake ‘CRDB Home Loans,’ wakati wa Maonesho ya Pili ya Sekta ya Nyumba  ‘Tanzania Homes Expo 2012 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mauzo wa CRDB. (Picha na Habari Mseto Blog)

 Baadhi ya Maofisa wa Benki ya CRDB walkiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonesho Maonesho ya Pili ya Sekta ya Nyumba  ‘Tanzania Homes Expo 2012 yaliyomalizika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mauzo wa CRDB, Theresia Lubogo, Meneja Mwandamizi Mahusiano ya Wateja wa benki ya CRDB Silas Katemi, Nirrah Chemchem, Neema Daniel na Ofisa Masoko wa CRDB, Ninael Munuo.
Meneja Mwandamizi Mahusiano ya Wateja wa benki ya CRDB, Silas Katemi (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Charles Kitwanga ya utaratibu mpya wa ukopeshaji pesa za ununuzi na ujenzi wa nyumba za makazi kwa wateja wake ‘CRDB Home Loans,’ wakati wa Maonesho ya Pili ya Sekta ya Nyumba  ‘Tanzania Homes Expo 2012 yaliyomalizika leo jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM, Tanzania

 BENKI ya CRDB imetambulisha utaratibu mpya wa ukopeshaji pesa za ununuzi na ujenzi wa nyumba za makazi kwa wateja wake ‘CRDB Home Loans,’ utakaowawezesha watu binafsi na waajiriwa kumiliki makazi bora na ya kisasa kwa riba ndogo. 

Akizungumza na Tanzania Daima wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Sekta ya Nyumba ‘Tanzania Homes Expo 2012, Meneja Mwandamizi Mahusiano ya Wateja wa CRDB, Silas Katemi, alisema kipindi cha ulipaji wa mkopo wa Home Loans ni kirefu hadi miaka 20. 

Aliwataka Wanzania kutembelea matawi ya CRDB yaliyo karibu yao ili kupata maelezo kuhusu CRDB Home Loans – utaratibu rahisi, wenye riba ya kuvutia na unaomuwezesha kila mteja wa benki hiyo, mwajiriwa na asiye mwajiriwa kumudu kuulipa taratibu tofauti na kampuni au mabeki mengine.

 “Miradi ya ujenzi wa makazi bora kwa Watanzania kwa sasa inahusisha kampuni mbalimbali kama unavyoziona hapa, ushindani huu umetusukuma sisi CRDB kuweka riba ndogo kati ya asilimia 16 hadi 20 ambayo itamvutia kila mmoja,” alisema Katemi.

 Katemi aliongeza kuwa, gharama za ujenzi kwa sasa ziko juu, hali inayowakwamisha wateja wengi kujenga makazi bora kwa awamu moja hivyo kufanya ujenzi wa ‘kuungaunga,’ lakini kupitia CRDB Home Loans, wateja watajenga na kununua mara moja, kisha kulipa taratibu. Tanzania Homes Expo 2012 ni maonesho ya pili kufanyika nchini, ambapo mwaka huu yalifunguliwa Ijumaa kwenye Viwanja vya Mlimani City na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na kushirikisha kampuni mbalimbali zinazojihusisha na sekta ya nyumba.

1 comment:

  1. I really like your blog.. veгy nice colοrs & theme.
    Diԁ you desіgn thiѕ wеbsite yourself οr diԁ уοu
    hiгe sοmeone to do it for you? Ρlz гeply aѕ
    ӏ'm looking to design my own blog and would like to find out where u got this from. many thanks
    My web page > prosper loans bbb

    ReplyDelete