Tuesday, December 4, 2012

JAMBO CONCERPT YAZINDUA GAZETI LA MATANGAZO LA DARMETRO


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concerpt Tanzania Limited, Juma Pinto (kushoto) akiwa pamoja na Meneja Matangazo wa Kampuni hiyo, Lightness Sirikwa na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Matangazo la DARMETRO, Yakobe Chiwambo wakati wa uzinduzi rasmi wa Gazeti hilo maalum kwaajili ya Matangazo litakalo kuwa likisambazwa bure jijini Dar es Salaam.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concerpt Tanzania Limited, Juma Pinto akizungumza kuhusiana na gazeti hilo jipya la Matangazo. Mbali na kuhusika zaidi na matangazo lakini pia litakuwa na habari za kibiashara na kutoka kila Jumatatu.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concept Tanzania Limited, Ramadhan Kibanike akitoa maelezo juu ya Kampuni hiyo na Magazeti na Majarida inayotoa hadi sasa kuwa ni Gazeti la Jambo Leo, Jambo Brands na sasa DARMETRO.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept Tanzania Limited, Ben Kisaka (kushoto) na Juma Pinto wakiwa na mmoja wa watu wa karibu kabisa na mdau wa Jambo Concept, Evance Aveva wakifuatilia uzinduzio huo leo katika mgahawa wa City Sport & Lounge uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa tasnia ya habari na Matangazo wakifuatilia uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment