Friday, December 14, 2012

KAMPUNI YA STARTIMES NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA YA DIGITALI


Kwa maelekezo ya ITU  kwamba  huduma za televisheni za utangazaji  kubadili kutoka Analojia na kwenda katika   mfumo wa digitali kabla ya Juni 17, 2015, lakini kwa nchi ya Tanzania tarehe ya  mwisho ya kubadili mfumo ni  Desemba 31, 2012.
Ili kuwa na uwezo wa kutekeleza mabadiliko haya  katika wakati, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) imeunda kampuni ya  Ubia na  kampuni ya Star Communication Network Technology Co. LTD ya  China, inayojulikana kama Star Media (Tanzania) LTD inayotumia jina la kibiashara la  STARTIMES. wajibu wa Kampuni hii ya Ubia na  ya kisasa, ni kuleta mapinduzi katika huduma za televisheni na utangazaji kwa njia  ya digitali na kutoa huduma za multiplex katika Tanzania. STARTIMES tayari imeshabadili na kuingiza katika mifumo ya digitali  mikoa saba  katika Tanzania Bara yaani Mwanza, Mbeya, Dodoma, Arusha, Moshi, Tanga na Dar es salaam. Kufikia  mwisho wa mwaka huu,kabla ya kubadili rasmi mfumo  mkoa wa Morogoro pia utaunganishwa katika mfumo wa digitali kama miko tajwa.
Inatarajia  pia  kujenga Kituo cha  kurushia cha kisasa katika eneo la Makongo kilimani ili kuboresha signal/urushwaji wa matangazo yetu  katika Mkoa wa  Dar es Salaam  na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani.
Kampuni ya Star Time vile vile inakusudia kubadili Zanzibar na tayari tumepata  leseni kwa ajili ya kujenga kituo cha televisheni na kupeleka huduma za mfumo wa digitali kabla ya tarehe ya kubadili (Switch –off) kama kila kitu kitakwenda kulingana na mipango yetu. Hata hivyo, mpango wetu ni kwamba Tanzania nzima lazima kubadilishwa kwenda kwenye mfumo wa digitali  mapema iwezekanavyo ili kila Mtanzania anaweza kufurahi ulimwengu wa digitali.

No comments:

Post a Comment