Monday, December 10, 2012

Mantra yapiga jeki kituo cha ushonaji cha Utete Songea




Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo (wapili kushoto) akibadirishana nyaraka za makubaliano na Mkuu wa Kituo chaUshonaji cha Utete Tailoring Mart kilichopo Songea, Mkoani Ruvuma Atnas Nyumbi (katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi cherehani ya kisasa itakayotumika kutengeneza sare za wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra .Picha na mpiga picha wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo (kushoto) akikabidhi cherahani ya kisasa kwa Mkuu wa Kituo chaUshonaji cha Utete Tailoring Mart Atnas Nyumbi (kulia)ambayo itasaidia kutengeneza sare za wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra .Picha na mpiga picha wetu. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo (wapili kushoto) akionyesha sare za wafanyakazi wa kampuni hiyo zinazotengenezwa na Kituo chaUshonaji cha Utete Tailoring Mart kilicopo Songea Mkoani Ruvuma wakati wa hafla fupi ya kukabidhi cherahani ya kisasa kwa Mkuu wa Kituo hicho Atnas Nyumbi (kushoto)mwishoni mwa wiki.Picha na mpiga picha wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo (kushoto) na Mkuu wa Kituo chaUshonaji cha Utete Tailoring Mart kilichopo Songe, Mkoani Ruvuma Atnas Nyumbi (kulia) wakitia sahihi hati za makubaliano zitakazowezesha kituo hicho kutengeneza sare za wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra .Picha na mpiga picha wetu.
Na mwandishi wetu , Songea


KAMPUNI ya Mantra Tanzania imeendeleza jitihada zake za kusaidia jamii inayoizunguka kwa kutoa cherehani yakisasa inayotumia mfumo wa komputa kwa Kituo cha Ushonaji cha Utete Tailoring Mart kilichopo mjini Songea , Mkoani Ruvuma.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi cherehani hiyo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanzania Asa Mwaipopo alisema kuwa kampuni yake imejizatiti kusaida kupunguza umasikini kwa kusaidia miradi mabali mbali ya maendeleo kwenye Mkoa huo wa Ruvuma.

Mwaipopo alisema tayari kampuni yake imesaini hati za makubaliano na Kituo cha Ushonaji cha Utete ambapo kituo hicho kitatengeneza sare (uniform) za wafanyakazi wa kampuni yake hali ambayo itasaidia kujenga uwezo wa kituo hicho.
 “Kampuni ya Mantra ina nia ya kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo kwakutambuma umhimu wa miradi hiyo katika kupunguza umasikini. Kwa lengo hilo, leo tunakabidhi cherehani ya kisasa kwa kituo hichi cha Utete na tunaamini jitihada zetu zitakuwa chachu ya maendeleo ya kituo hiki.

Mwaipopo alisema cherehani hiyo imetolewa kwa mtindo wa mkopo wa mzunguko (Revolving Fund) na kusema kuwa pesa itakayopatikana itasaidia kuendeleza washonaji wengine mkoani humo.

“Atalipia kwa utaratiu wa kazi ambazo tutakuwa tukimpa kwa makato ya taratibu. Pesa ambayo itapatikana itasaidia kuinua washoinaji wengine. Ni matumaini yangu kuwa cherehani hii itatumika kwa matumizi sahihi iliiweze kuka muda mrefu ,” alisema Mwaipopo.

Maipopo alisema kuwa kampuni yake inatakribani wafanyakazi 150 na kusema kuwa idadai hiyo itaongozeka maradufu kufikia wafanyakazi 1500 kipindi Mradi wake wa Urani wa Mto Mkuju utakapoanza.
“Ni matumaini yetu kuwa sare za wafanyakazi wote hao zitatengenezwa na kituo hich cha Utete. Hii sikazi wa mtu mmoja kwahiyo lazima kituo hiki kiaajiri washonaji wengine. Ni matumaini yetu kuwa wananch watachangamkia fursa zitakazopatikana,” alisema.

Naye Mkuu wa Kituo hicho cha ushonaji cha Utete Atnas Nyumbi alisema msaada huo umekuja muda muafaka na kuahidi kutumia cherehani hiyo vizuri ilikupata mafanikio makubwa zaidi.
 “Tunashukuru Kampuni ya Mantra kwa kuwa na imani na kituo chetu. Tunaahidi kutumia cherehani hii vizuri ilituweze kupata mafanikio na kusonga mbele,” alisema Nyumbi.

Kampuni ya Mantra Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusadia miradi mbali mbali ya maendeleo kwenye Mkoa wa Ruvuma ikwemo miradi ya afya, elimu, utunzaji wa mazingira pamoja na michezo.

No comments:

Post a Comment