Monday, December 10, 2012

MH. KITWANGA AHITIMISHA ZIARA KATIKA VIWANDA NA MAHOTELI JIJINI NA KUKEMEA WANAOCHAFUA FUKWE ZA BAHARI


strong>
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa tatu kulia) akiwasili katika Kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha Shelys kilichopo Mwenge jijini Dar huku akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ( wa pili kulia), Mkurugenzi wa Kurugenzi ya kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga na Wataalamu wa Kitengo cha Mazingira kutoka katika Wizara yake katika muendeleo wa ziara za kushtukiza Viwandani kukagua mfumo wa mazingira ya maji taka yenye kemikali katika viwanda hivyo kama unaendana na viwango vilivyowekwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akieleza dhumuni la ziara yake katika kiwanda hicho kwa Afisa Rasilimali watu wa Kiwanda cha dawa cha Shelys Bw. Nissa Mwaipiana (kulia).
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akitoa maelezo kwa Naibu Waziri na Ujumbe wake.
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akimwongoza Mh. Charles Kitwanga kwenda kukagua sehemu ya kutibu maji taka yenye kemikali.
Mwendesha Mashine wa Kiwanda hicho Bw. Patrick Mapunda (mwenye koti) akitoa ufafanuzi Kwa Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga wa namna wanavyokusanya na kuyatibu maji taka yanayotokana na uzalishaji kiwanda hapo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa maagizo wa NEMC baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho kutofikia ubora unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga(wa pili kulia) akiongozwa na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden (kulia) kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho. Country PAC Manager wa kiwanda hicho Bw. Evans Mlewa (wa pili kushoto) na kurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden akitoa Maelezo kwa Mh. Kitwanga juu ya Mitambo Mipya ya Kisasa yenye kiwango cha Kimataifa kwa ajili ya kutibu maji taka katika Kiwanda hicho.
Mh. Kitwanga na Ujumbe wake ukitizama Bwawa la Samaki linalotumika kufanyia majaribio ya maji taka ambayo yamekwisha safishwa kwa ajili ya matumizi mengine kiwandani hapo.
Mh. Charles Kitwanga (kulia) akitoa maoni yake baada ya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda cha CocaCola na kuridhishwa na utaratibu unaotumika katika uzalishaji wa bidhaa zao na mfumo wa kuhifashi maji taka na kuyasafisha kwa njia ya kisasa na kuitaka kampuni hiyo iwe mfano wa kuigwa na iwe Mwalimu kwa Makampuni mengine.
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Soda cha CocaCola Bw. Basil Gadzios (katikati) akitoa shukrani kwa Mh. Naibu Waziri na kuahidi kutoa ushirikiano wa kitaalam kwa viwanda vingine juu ya utunzaji wa maji taka na namna ya kuyasafisha kisasa kuepuka kuharibu Mazingira na kuongeza kuwa Kampuni ina mkakati kabambe kwa mwaka 2013 kutengeneza ajira kwa vijana ambapo inakusudia kujenga vituo katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya vijana kukusanya chupa za plastiki zinazotokana na kiwanda hicho kwa ajili kuzalishwa upya.
Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha CocaCola Bw. Basil Gadzios na Ujumbe wa NEMC na Maafisa wa Wizara yake.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa pili kushoto) akiwasili katika Hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam kujionea jinsi Hoteli hiyo iliyopo ufukweni mwa bahari inavyotunza mazingira yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya White Sands Alwyn Kellerman na Afisa Mazingira wa Hoteli hiyo Bi. Linda Mbuya.
Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli hiyo akifunua chemba inayopitisha maji taka kwa ajili ya kukaguliwa na jopo la wataalam kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara. Katika ukaguzi huo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga hakuridhishwa na jinsi hoteli hiyo inavyoendesha mfumo wake wa maji taka na kuagiza timu ya wataalam kutoka NEMC kufanya ukaguzi upya wa mifumo hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View Bw. Nicholas Oyieko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mh. Kitwanga (wa pili kushoto) jinsi hoteli hiyo inavyotunza mazingira na namna inavyodhibit mfumo wake wa maji taka kuhakikisha kwamba haileti madhara.
Hii ni sehemu iliyoko pembeni ya Hoteli ya Giraffe ambayo mmiliki wake hafahamiki ambayo imewekwa uzio na kufanya bahari kushindwa kupumua vizuri na kusababisha mkusanyiko wa uchafu unaodaiwa kutuama mahali hapo tangu mafuriko ya hivi karibuni yaliyoikumba jiji la Dar es Salaam. Naibu Waziri ameamuru muhusika kutafutwa mara moja na kupigwa faini na kuamuriwa kuondoa vifusi hivyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na ujumbe wake wakiangalia eneo hilo.

No comments:

Post a Comment