Monday, December 3, 2012

PROFESIONAL KIBAO NDANI YA NDONDO DAR ES SALAAM


Mshambuliaji wa Mpumalanga Adam Kingwande (Anachezea African Lyon)  mwenye mpira akijaribu kumtoka mshambuliaji wa Vuguvugu Husein Kicheche (Anachezea Bandari ya Kenya) kwenye mchezo wa fainali ya mashindano ya jezi uliochezwa juzi uwanja wa Chuo cha Bandari, Vuguvugu ilitwaa kombe baada ya kuifunga Mpumalanga mabao 4-2





Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Tandika wilaya ya Temeke akikabidhi zawadi ya mbuzi nahodha wa timu ya Mpumalanga amabo ni washindi wa pili wa mashindano ya jezi yaliyokuwa yameandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kata ya Tandika kwenye uwanja wa Chuo cha Bandari, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Kimataifa anayechezea Bandari ya Kenya inayoshiriki ligi kuu nchini humo Husein Kicheche jana aliisaidia timu ya mtaani kwake ijulikanayo kama Vuguvugu kutwaa kombe la jezi lililochezwa uwanja wa Chuo cha Bandari.


Mchezo huo ambao ulikuwa wa fainali ya mashindano ya kuwania jezi uliandaliwa na Umoja wa Vijana Kata ya Tandika wilaya ya Temeke na ulizikutanisha timu zaidi ya 30.

Fainali ilichezwa katti ya Vuguvugu na Mpumalanga, mchezo ambao ulivuta hisia za mashabiki kiasi cha kujaza uwanja wa Chuo cha Bandari kutokana na timu zote kuwa na wachezaji wa wanaocheza ligi kuu Bara na Zanzibar.

Timu ya Vuguvugu ambayo ilikuwa ikicheza mchezo wa kasi iliifunga wapinzani wake timu ya Mpumalanga mabao 4-2.

Mabao ya Vuguvugu yalifungwa na Babu Deo dakika ya 8 ya mchezo baada ya kupokea pasi toka kwa Husein Kicheche na la pili lilifungwa na Oseja Said dakika ya 30.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana iliwachukua dakika mbili kuongeza bao la tatu lililofungwa na Kimbu Musa anayechezea Toto African kwa shuti la mbali na karamu ya mabao ilihitishwa na Mponda Nurdin dakika ya 78.

Mpumalanga walipata bao la kwanza kwa njia ya penalti lililofungwa na Adam Kingwande dakika ya 58 na bao pili lilifungwa na Muhaji Kampala dakika ya 82.

Wachezaji wanaochezaji ligi kuu wamekuwa wakichezea timu za mtaani kwa kipindi hiki cha mapumziko.

Baada ya mchezo kumalizika mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Tandika alitoa zawadi ambapo timu ya Vuguvugu walikabidhiwa seti ya jezi na Mpumalanga walipewa zawadi ya mbuzi.

Pia aliwaasa wachezaji kutumia michezo kama ajira hivyo nidhamu ni muhimu ili kufikia malengo yao.
"Mnatakiwa mcheze michezo mkijua ndio ajira yenu hivyo nidhamu ni muhimu ili kufikia malengo mliojiwekea", alisema.

No comments:

Post a Comment