Monday, December 3, 2012

ROSE MUHANDO KUTAMBULISHA MPYA KUPITIA TAMASHA LA SHANGWE ZA KAGERA



MWIMBAJI maarufu wa muziki  wa Injili nchini, Rose Muhando amewataka wadau kujitokeza kwa wingi katika tamasha la ‘Shangwe Kagera’ linalitarajiwa kufanyika Desemba 9 kwenye Ukumbi wa Linas mjini Bukoba na uwanja wa Kaitaba.
Muhando na Enock Jonas ‘Zunguka’ watapamba katika maalum la kuchangia watoto yatima lenye lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika maisha magumu. 
Akizungumzia tamasha hilo Rose alisema amejiandaa kusherekea  Uhuru kwa aina yake tofauti na watu wengi walivvozoea kwa kuwashirikisha watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. 
“Nimefurahi kupata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hili la aina yake hasa katika  mkoa wa Kagera ambapo itakuwa mara ya kwanza kuonekana live katika mji wa Bukoba”, alisema . 
Muhando aliwamba wananchi wa Bukoba kufika kwa wingi katika tamasha hilo la kipekee katika ukuonyesha moyo wa upendo kushirikiana na kusaidia jamii ya watu wengine wasio jiweza.
Alisema kupitia tamasha hilo anatarajiwa kuwapa uhondo wa nyimbo zake za zamani sambamba na kutambulisha nyimbo zake mpya ambapo wakazi wa huko watapata fursa ya kuzisikiliza kwa mara ya kwanza. 
 Naye Zunguka amewataka wakazi wa Kagera kukaa mkao wa kula kwa ajili ya tamasha hilo na watarajie kupata burudani ya kutosha na ya kipekee kutoka kwake  ambayo itawajenga roho ya imani, kupendana na kusaidia watu yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili nao waweze kufaraia maisha. 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kuwataka wadau kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Aliongeza kuwa mbali ya wasanii hao, pia tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka  bendi ya muziki ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya wanakwaya  wa makanisa mbalimbali na  kikundi cha watoto yatima.

No comments:

Post a Comment