Thursday, December 6, 2012

WANANCHI WAJITOKEZA VIWANJA VYA KARIMJEE KUTOA MAONI KATIBA MPYA



Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Jospeh Warioba (kulia) na Wajumbe wengine bw. Joseph Butiku na Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam jana jioni.

Bi. Martha Pius (41), mfanyabiashara mkazi wa Mwanza akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika jana jioni katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Bw. Steven Munisi (20), mwananfunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika jana jioni katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Bi. Verda Savella (32) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika jana jioni katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Bw. William Ndiye Keiya (31), mkazi wa Ungungo Kibangu jijini Dar es Salaam akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika jana jioni katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakijaza maoni yao katika fomu maalum kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam jana jioni.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni yao kuhusu Katiba Mpya uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam jana jioni.

No comments:

Post a Comment