Monday, January 7, 2013

Mpango wa kusomesha mtoto wa mkulima wa Zabibu Dodoma



DAR ES SALAAM, Tanzania

Mpango huu wa kusomesha watoto wa mkulima unaojulikana kama “Zabibu na shule kwanza” ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 01 Julai 2011 Bungeni Dodoma na  Spika wa bunge la Tanzania, mama  Anna Makinda.
Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha familia za wakulima walio kwenye mkataba na TDL wanafaidia na kazi za wazazi wao kwa kusaidia watoto wa familia hizo kwenda shule, kupunguza idadi kubwa ya watoto wanaoshindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na kukosa pesa za kulipia  ada na mahitaji muhimu ya shule kutoka kwa wazazi ama walezi wao ambao ni wakulima wa zao la zabibu.

TDL itakuwa imewapunguzia mzigo mkubwa na kuwapa wakulima hawa muda muafaka wa kujitatiti zaidi katika shughuli za  kilimo cha zabibu ili kuziwezesha familia zao kujikimu vizuri kimaisha.
Mradi huu ulianza na watoto kumi (10), na mwaka jana tukaongeza watoto ishirini (20) na ni matarajio kuwa mwaka huu idadi ya watoto watakaopewa ufadhili itakuwa wanafunzi ishirini (20), hivyo kufikisha idadi ya wanafunzi wanaosomeshwa na mpango huu kuwa wanafunzi hamsini (50).  

TDL kama kampuni tunaamini kuwa, uwekezaji kwenye elimu na pia kumsomesha mtoto  ni kukuza uchumi wa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment