Burudan Mwanzo - Mwisho

Thursday, January 24, 2013

MPIGA GITAA LA BESS MSONDO NGOMA AAGA DUNIA


 

Marehemu Ismail Mapanga, enzi za uhai wake.

MPIGA gitaa la besi wa bendi kongwe ya Msondo Ngoma, Ismail Mapanga, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo, katika Hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam na kuacha pengo kubwa katika bendi hiyo.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Said Kibiriti, alisema taarifa za msiba wa mwanamuziki ni nzito kwao, huku akitarajiwa kuzikwa leo saa saba mchana.

Kibiriti alisema kifo cha Mapanga ni pigo kubwa kwa bendi yao, hasa kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki wa dansi, akiwa na Msondo Ngoma.
Super D (Mnyamwezi) at 11:25 PM

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version
Powered by Blogger.