Saturday, January 12, 2013

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKAGUA MRADI WA BARABARA YA GONGO LA MBOTO JIJINI DAR LEO


Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa (katikati) akizungumza na wakandarasi wanaoshughulikia upanuzi wa barabara ya Nyerere kuanzia makutano ya uwanja wa ndege kuelekea Gongo la Mboto ambapo amesema kwa ujumla barabara inatanuliwa kutoka barabara mbili kuwa barabara tatu na kuchimbwa mitaro ya mvua ili maji yaliyokuwa yakiharibu barabara yaweze kupata njia.Amesema ukubwa wa kazi nzima ni kilomita 1.6 utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwa mradi huo unasimamiwa na wakala wa barabara yaani TANROADS. Aidha Mstahiki Meya ameitaka serikali ya kata kumsaidia mkandarasi kuondoa wafanyabiashara ambao wapo maeneo ya barabara ili kazi iweze kufanyika kwa wakati kwa kuwa kazi hii inatakiwa kuisha mwezi Mei mwaka huu. Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto Bw. Moshi Mwaluko na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki.
Pichani juu na chini ni Injinia Eliseus Mtenga (katikati) kutoka TANROADS Dar akitoa maelezo mafupi kwa Mh. Mstahiki Meya wa Ilala juu ya mradi wa upanuzi wa barabara ya kuelekea Gongo la Mboto kuanzia Ukonga Mombasa hadi njia panda ya Kiltex na marekebisho ya eneo korofi karibu na Sekondari ya Pugu ambapo amesema lengo ni kupanua barabara kwa Mita 3.0 kila upande ili kuwezesha njia tatu za magari kupatikana.
Hii ni awamu ya tatu katika upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili hadi tatu ambapo awamu ya kwanza ilihusisha Kilometa 1.8 na Awamu ya pili Kilometa 2.5 zilishakamilika. Kushoto ni Injinia Eliamin Tenga wa TANROADS na kulia ni Site Engeneer wa mradi huo Godson Tenga.
Mstahiki Meya Jerry Silaa (wa pili kushoto) akiongozana na Wakandarasi wa TANROADS pamoja na viongozi wa Kata ya Gongo la Mboto kukagua mradi wa barabara hiyo.
Injinia Eliseus Mtenga (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa Mstahiki Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea na ukaguzi wa barabara ya kuelekea Gongo la Mboto kuanzia Ukonga Mombasa hadi njia panda ya Kiltex yenye urefu wa Kilometa 1.6.
Pichani Juu na Chini ni Muonekano wa Barabara ya Kuelekea Gongo la Mboto kuanzia Ukonga Mombasa hadi Njia Panda ya Kiltex ikiwa kwenye matengenezo ya kuweka mifereji ya kupitisha maji ambayo yamekuwa yakiathiri barabara kipindi cha Mvua.
Injinia Eliseus Mtenga akiendelea kutoa maelezo ya mradi huo kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto.

No comments:

Post a Comment