Sunday, January 6, 2013

NDEGE MEDICS YAKABIDHI AMBULANCES ZA KISASA KWA HOSPITALI YA AGA KHAN KWA AJILI YA MRADI WA KUBORESHA AFYA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO TANZANIA

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania



Head of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis Nazrani.
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.
Aidha amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya kisasa.
Pichani Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Medics, Hospitali ya Aga Khan na waandishi wa habari walioshuhudia tukio la makabidhiano hayo.

Baadhi ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa rasmi leo kwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar ikiwa ni sehemu ya mradi Endelevu utakaohusisha Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa ajili ya kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto.

No comments:

Post a Comment