Thursday, January 24, 2013

RC IRINGA ATOA RAI KWA WANAHABARI NCHINI KUANDIKA HABARI ZA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA


Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Dr.Christine Ishengoma akifungua mafunzo ya siku moja ya tume ya haki  za binadamu na utawala  bora yanayotolewa kwa  wanahabari  wanachama wa klabu ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) na kufanyika katika ukumbi  wa Maktaba ya mkoa.
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Ishengoma wa tatu  kulia akiwa na viongozi mbali mbali  wa serikali na wanachama  wa IPC ,kutoka  kulia ni mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo, mkuu  wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba ,mkuu  wa mkoa wa Iringa Dr Ishengoma, Afisa uchunguzio mkuu wa haki za binadamu na utawala bora Shoma Philip  ,meya  wa manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi , Afisa uchunguziwa haki za binadamu na utawala bora  Nancy Ngula   na katibu mtendaji  wa IPC Francis Godwin
Katibu  mtendaji wa IPC akitoa utambulisho  wa  wanachama na kutoa neno la utangulizi juu ya mafunzo hayo. 
 MKUU  wa mkoa wa Iringa Dr  Christine Ishengoma awataka  wanahabari nchini  kujikita katika uandishi  wa habari za  haki za binadamu na utawala bora ili kuiwezesha jami kujua haki na wajibu wao katika maisha ya kila siku.
 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr  Christine Ishengoma alitoa rai hiyo leo katika ukumbi  wa Makitaba ya mkoa  wakati akifungua mafunzo kwa waandishi  wa habari wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) juu ya  haki za binadamu na utawala bora .
“Kupitia mafunzo haya, nendeni mkawasaidie wananchi kujua haki zao pamoja na utawala bora ili waweze kuwajibika pale wanapotakiwa kuwajibika msiishie  kuandika habari za kuwagonganisha viongozi na  wananchi pekee "amesema Ishengoma.
Amessema ili jamii iweze kujua haki zao ni lazima waandishi waelimishwe vizuri kwa kuwa wao ndio wasambazaji wa elimu na taarifa kwa jamii.
“Wanahabari ni muhimu sana kwa nchi yoyote ile duniani. Hii ni kwamba mwanahabari ni chombo muhimu katika usambazaji wa elimu kwa jamii na wao ni kiungo kikubwa kati ya serikali na jamii katika mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mwana habari ni mtu wa kuheshimiwa kwa kuwa ni watu wakutegemewa” amesema.
Nance Ngula afisa uchunguzi na utawala bora ambaye alikuwa mkufunzi ameseme kila mtu anahusika katika suala zima la haki za binadamu na utawala bora kwa kuwa ndio walengwa wa masuala hayo.
Amesema ukiukwaji wa haki za binadamu unaweza kufanywa na mtu yeyote yule bila aidha kwa kutumia wadhifa alio nao au kwa makusudi na kutowajibika katika nafasi.
Ngula aliwata waandishi kuwa na utaratibu wa kuzifikia jamii na kujua changamoto wanazokabiliana nazo na kutumia nafasi walizo nazo kwa kuwasaidia kuondokana nazo aidha kwa kutumia elimu yao au kutafuta msaada mbadala.
Naye Shoma Philip afisa uchunguzi mkuu wa haki za binadamu na utawala bora alisema utawala bora ni pamoja na kuzingatia haki zote za binadamu katika ngazi zote bila kujali umri.
Amesema hata utoaji mimba ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa unakiuka haki ya kuishi ambayo kila mtu anatakiwa kuipata.
“Utawala usiozingatia haki za binadamu hauwezi kuitwa utawala bora kwani ili haki ziweze kuzingatiwa lazima kuwepo na utawala bora” amesema.
Amesema kila wakati migogoro mingi inasababishwa na ukosefu wa utawala ulio bora kwa kuwa haki za binadamu zinakuwa hazithaminiwi.
Aidha amesema jamii pia ina wajibu wa kutimiza yale ambayo yanawapasa ili kusiwe na migongano na malalamiko kwa upande wao.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na kuratibiwa na idara ya haki za binadamu na utawala bora katika serikali.

No comments:

Post a Comment