Thursday, January 10, 2013

WAZIRI MKUU PINDA NA BIBI SHAMBA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo zaidi kuhusu aina ya mbegu ya mahindi iliyotumika kutoka kwa Bi. Grace Hokororo ambaye ni Bibishamba wa kata ya Itenka wakati alipokuwa akikagua shamba darasa analolisimamia kwenye kijiji cha Itenka wilayani Mlele, Katavi, Januari 6, 2013. Alifurahia kazi yake na kuahidi kumpatia pikipiki imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia. PICHA ZOTE/OFISI YA WAZIRI MKUU

Bibishamba wa kata ya Itenka, Bi. Grace Hokororo akimshukuru Waziri Mkuu Mizengo kwa kufanya ukaguzi kwenye shamba darasa analolisimamia analolisimamia katika kijiji cha Itenka wilayani Mlele, Katavi. Aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.

Bibishamba wa kata ya Itenka, Bi. Grace Hokororo akipokea zawadi ya sh. 305,000/-  kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambazo zilichangwa papo hapo na watu alioandamana nao ili kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye shamba darasa. Wa pili kulia ni Bw. Joseph Laurent anayesimamiwa na bibishamba huyo ambaye shamba lake lilikaguliwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha Itenka  wilayani Mlele, Katavi. Pia aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia.

No comments:

Post a Comment