Tuesday, January 8, 2013

WAZIRI WA FEDHA AZINDUA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU MIL. 49, UYUI, TABORA


Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia. Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa akikata utepe wa uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyogharimu milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui wakati Waziri huyo alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kushoto ni Mbunge wa Jimbo Tabora Kaskazini Mamlo Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia wa Mbola Dkt Gerson Nyadzi.

PICHA na GCU - HAZINA

No comments:

Post a Comment