Tuesday, January 29, 2013

ZIARA YA PINDA MTWARA VIKWAZO VITUPU MADIWANI WAKATAA GESI KUSAFIRISHWA, Mkutano waisha bila kukubaliana. Ashindwa kuzungumza na waandishi wa habari. Mkutano walindwa na JWT na Polisi.



Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho. Kwa sasa anakula chakula na kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara kitafuatia. Kutokana na kuwepo kwa makundi katika Kamati ya siasa ya CCM mkoa, wabashiri wengi wanasema kikao hicho kitakuwa na mvutano mkali.
Dondoo Muhimu
*Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi kwenda Dar.
*Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye.
*Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja  Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka yake  kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara vijijini kuunga mkono suala la gesi kusafirishwa kwenda Dar, Madiwani wa Mtwara vijijini wamesema hawakushirikishwa.
   *Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
   *Waziri Mkuu kutumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi bomba liende Dar
   *Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu.
   *Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na Usalama wa Taifa.
   *Hawa Ghasia arudishwa uwanja wa Ndege JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa.
    *Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema      wao ndio chanzo cha vurugu.

No comments:

Post a Comment