Friday, January 4, 2013

ZITTO KABWE: Maandamano dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji.


ZittoKabwe
 
Dar inachangia asilimia 80 ya mapato. Kitovu cha Uchumi. Darinachangia 90% ya ufisadi.
Uti wa mgongo wa ufisadi nchini”
Malumbano kati ya wananchi wa Mtwara na Serikali kuhusu matumizi boraya utajiri wa nchi yameendelea kwa takribani wiki moja sasa.Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Nishati na Madinikuwaita Watanzania wa Mtwara Wahaini, wapuuzi na watu hatari, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania naye aliingia kwenye mjadala huo kwakuonya watu wanaowaunga mkono watu wa Mtwara na kuwaita watuwanaotafuta umaarufu wa kisiasa na wanaotaka kugawa nchi.Siku moja baada ya hotuba ya Rais, Waziri wa Nishati na Madini alifanyamkutano na waandishi wa habari kueleza suala lile lile ambalo bosi wakealilielezea usiku wa kuamkia mwaka mpya 2013. Hii ni dalili ya Serikalikuweweseka.Katika kauli ya Serikali, ambayo haikuwa na jipya zaidi ya wimbo ule ule wa
 ‘kugawa nchi’ ‘umaarufu wa kisiasa’ nk,
Serikali ilitaka kuonyesha ummakuwa watu wa Mtwara hawana shukurani.Kwamba miaka yote toka Uhuru watu wa Mtwara wamekuwa wakilishwana Pamba, Kahawa, Chai, Tumbaku, Sukari, Kidatu nk. Kwamba watu waMtwara na Lindi hawakuchangia hata kidogo kwenye hazina ya Taifa. Hivyowao kupigia kelele gesi yao ni uchoyo na roho mbaya na kukosa shukurani.
Kauli ya Serikali ni kauli ya chombo kinachoendelea kukosa ‘legitimacy’ ya
kuongoza taifa. Ni kauli ya kukata tamaa. Ni kauli hatari sana dhidi yaWatanzania waliojitolea damu kulinda uhuru wa nchi yetu.Moja, Serikali katika kauli yake haitaji kabisa kwamba toka Uhuru watu waMtwara na Lindi wamekuwa wachangiaji wakubwa sana katika uchumi waTaifa kupitia zao la Korosho.Takwimu za Uzalishaji wa Korosho zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka1965 mpaka 2011 Korosho imeliingizia Taifa fedha kigeni jumla ya dola zaKimarekani 4.58 bilioni ( Cashewnuts Sub-sector study 2003, Hali yaUchumi 2012, Cashewnuts Tanzania Report 2010).Katika Mwaka wa Uchumi unaoishia Novemba 2012, Korosho imeliingiziaTaifa jumla ya dola za Kimarekani 151 milioni. Katika mwaka 2011 zao hilililiingiza dola 130 milioni wakati Pamba iliingiza dola 53 milioni tu.Licha ya Zao la Korosho kuingiza fedha hizi za kigeni (sawa ni shilingitrilioni 7.2) kwa nchi mikoa ya Lindi na Mtwara ipo miaka 50 nyumakimaendeleo kulinganisha na mikoa mingine ya Tanzania.Serikali inataka kufuta historia ya mchango wa zao la Korosho kwenyeuchumi wa nchi yetu kwa sababu ya uroho wa gesi asilia. Kwa nini kaulirasmi ya Serikali haijataja Korosho kabisa?Kauli hii ilipitishwa na ngazi zote za Serikali? Mawaziri wa Serikaliwanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara walikubali kauli kama hii itoke dhidiya wananchi wao wanaoteseka na zao la Korosho miaka nenda miaka rudi?Pili, Serikali imesahau kabisa mchango wa watu wa Lindi na Mtwara katikaulinzi wa Taifa letu. Moja ya sababu ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwanyuma kimaendeleo ni juhudi za ukombozi wa kusini mwa Afrika.Kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji ilikuwa Nachingwea. Kambi yaFrelimo iliwekwa kwenye Shamba la Mkonge kilometa 17 tu kutoka mjiniNachingwea ambapo ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa Msumbiji. RaisSamora Machel, Rais Joaqim Chissano na Rais Guebuza waliendeshamapambano kutoka kusini mwa Tanzania.Makaburu wa Afrika Kusini na Wareno walikuwa wanashambulia nchi yetu
na mikoa hii miwili ya Lindi na Mtwara ikawa ‘buffer zone’. Wakati Dar es
Salaam inaendelea kwa kila aina ya maendeleo, mikoa ya Lindi na Mtwarailikuwa inalinda ili wanaoishi Dar es Salaam na mikoa mingine waishi waamani na starehe. Serikali inapimaje mchango huu wa mikoa hii?
Tunaipima kwa fedha? Uroho wa gesi asilia kuzalisha umeme wakufurahisha walalaheri asilimia 14 nchini ndio inaifanya Serikali kusahau
kabisa ‘sacrifice’ ya watu wa Mt
wara katika kulinda uhuru wa Taifa letu?Tatu, Serikali inasema lazima bomba lije Dar es Salaam kwa sababu Darndio inazalisha asilimia 80 ya Mapato ya Serikali. Kwanza huu ni uwongo.Ni aibu Serikali kujitetea kwa uwongo. Dar es Salaam ni kituo tu chakukusanyia mapato ya Serikali. Uzalishaji mkubwa wa nchi yetu wenyekuzalisha kodi unafanyika nje ya Dar es Salaam.Walipa kodi wakubwa wengi Ofisi zao Kuu zipo Dar es Salaam lakiniuzalishaji wao unafanyika nje ya Dar es Salaam. Serikali itoe orodha yawalipa kodi wakubwa 100 tuone uzalishaji halisi wa mapato hayounafanyika wapi.
Hata hivyo inawezekana kuwa ikawa kweli Dar es Salaaminakusanya asilimia 80 ya mapato ya nchi.Basi na tuseme Dar es Salaam inachangia asilimia 90 ya ufisadiwote nchini. Kashfa zote kubwa za Ufisadi zinafanyika Dar esSalaam na fedha nyingi za ufisadi zinatumika Dar es Salaam.
 Mwisho, maandamano ya watu wa Mtwara ni kielelezo tosha kwamba watuwa mikoa ya Lindi na Mtwara wamechoshwa na longolongo za Serikali.Wananchi wa Mtwara na Lindi wanataka Uwajibikaji wa Serikali kuhusuutajiri wa nchi. Mtanzania yeyote mwenye tahadhari ya nchi yetu kutokuwana laana ya rasilimali ataungana mkono na watu wa Lindi na Mtwara kudaimaendeleo.Nilitoa mfano wa Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yotetani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega.
Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milionikuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997).Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuzadhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni.Kabla Serikali haijawaita watu Mtwara wahaini, wapuuzi na watuhatari, iwaambie watu Watanzania kodi kiasi gani imekusanywakutoka mgodi huu katika kipindi cha miaka 14.Mpaka mwaka 2008, kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bomani,kampuni hii ilikuwa imelipa mrahaba wa dola 11 milioni na kodi

No comments:

Post a Comment