Monday, February 4, 2013

BONDIA WA ZAMANI MUHAMMAD ALI YUPO KITANDANI AKISUMBILIWA NA MARADHI



Bondia Muhammad Ali akimdondosha chini mpinzani wake katika moja ya mapambano yake

LONDON, England
Rahman Ali ndugu wa kuzaliwa wa Muhammad, amefichua: “Ndugu yangu hawezi kuongea, hawezi hata kunitambua mimi. Yuko katika hali mbaya kwa kweli. Ali anaumwa sana”
NDUGU wa kuzaliwa wa bondia wa zamani Muhammad Ali, 71, Rahman Ali amesema kuwa hali ya kaka yake ni mbaya na anapigania maisha yake kujikoa na kifo, huku siku zake za mwisho zikizua shaka, simanzi na vilio kwa mke wake.
Rahman, 69, amesisitiza kuwa homa pekee si sababu inayoyaweka hatarini maisha ya nduguye, bali shambulio la moyo lililochukua fahamu zake lina mchango mkubwa wa kuhitimisha zama za mkongwe huyo.
Akiwa katika mahojiano juu ya hali ya kaka yake, Rahman alidondosha machozi chini kwa uchungu na kusema yeye binafsi angependa kumuona kaka yake akifariki sasa, ili kumuepushia na matatizo anayokumbana nayo.
Rahman alifichua kwamba: “Ndugu yangu hawezi kuongea, hawezi hata kunitambua mimi. Yuko katika hali mbaya kwa kweli. Ali anaumwa sana.
“Inaweza kuwa miezi, inaweza kuwa baada ya siku kaddhaa. Mimi sijui kama atafika majira ya joto. Yuko katika mkonono ya Mungu. Tunatarajia kuona Mungu akimponya.
“Aliniambia hapo kabla ya kuzidiwa kwamba haumwi na hasikii maumivu yoyote. Alinyanyua mkono wangu na kunipa wasiwasi kwa kuniaga, ‘Rahman, nimefanikiwa katika kila kitu na nimekamilika kimafanikio. Usilie kwa ajili yangu, mimi siumwi na sina maumivu yoyote,’
“Ali ataenda peponi, hakuna shaka juu ya hilo. Kama atakufa na kuzikwa kesho, mataifa yote na watu wote duniani watageuka na kuungana kwa ajili yake. Ali alimgusa na kumvutia kila mmoja kuanzia maskini hadi matajiri.
“Nampenda ndugu yangu kuliko mtu yeyote. Katika watu wote maarufu walio hai, huyu ni bora zaidi yao. Kila mmoja anajua kwamba Muhammad Ali. Yeye yuko juu pamoja na Yesu Kristo.
“Mimi nalia kwa sababu nina machungu juu yake, ananivunjaa moyo wangu. Nina matumaini ya ya kumuona tena akiwa hai, lakini ninaweza tu kutumaini.”
…….The Sun……

No comments:

Post a Comment