Monday, February 25, 2013

Extra Bongo yaipiga 'Tafu' Free Media Queens




Mwakilishi wa Extra Bongo, Super Nyamwela akimkabidhi fedha taslim sh 200,000 kwa mwandishi  wa Kampuni ya Free Media, Clezencia Tryphone 'Tasha' kwa ajili ya maandalizi ya michunao ya NSSF Cup hafla hiyoilifanyika katika ukumbi wa Meeda Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Na Mwandishi Wetu

KATIKA hatua zaidi za kufanikisha maandalizi ya michuano ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF Cup), Bendi ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, imedhamini katoni 33 za maji ya Kilimanjaro kwa timu ya wanawake ya Netboli ya Free Media Queens.

Akikabidhi udhamini huo wenye thamani ya sh 200,000, mwakilishi kutoka Extra Bongo Super Nyamwela katika ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam juzi usiku alisema, bendi yao imeamasika mara baada ya Free Media Queens kuhitaji sapoti yao katika suala muhimu la kimichezo.

Nae Mmiliki wa bendi hiyo, Ally Choki alisema, sapoti hiyo wameitoa kwa moyo mkunjufu kutokana na umuhimu wa michuano hiyo inayojenga afya zaidi na kudai kuwa, mara baada ya kupata ombi hilo hakusita kusapoti.

“Michuano hii ni mizuri sana, nawapongeza NSSF kwa kuona umuhimu wa waandishi kama mimi nilivyoona na kutoa sapoti walau kidogo kwa timu hii ya Free Media Queens ili iweze kufanya vema maandalizi yake,”alisema Choki.

Mbali na sapoti hiyo, Choki ameitaka timu hiyo kujipanga kikamilifu ili iweze kufanya vema katika michunao hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi Machi 9 katika uwanja wa TCC Chang’ombe pamoja na DUCE Jijini Dar es Salaam.

Michuano ya NSSF, inashirikisha timu mbalimbali za wanahabari kutoka Bara na Visiwani, ikiwa na lengo la kudumisha amani na undugu katika kazi.

Katika hatua nyingine, Choki amewataka wasichana kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu za kushiriki shindano la Kigoli wa Manywele linalotarajiwa kutimua vumbi hivi karibuni, ambapo fomu za ushiriki zinaanza kutolewa leo katika ofisi za Manywele na Extra Bongo.

“Wanadada wakati ni wenu jitokezeni kwa wingi, kuchukua fomu zinazoanza wiki ijayo, ili muweze kuibuka na gari la kisasa kwa mshindi wa kwanza, wa pili makochi na wa tatu atapata zawadi kali ambayo nitaitoa mimi binafsi,”alibainisha Choki.

Aliongeza kuwa, Bendi yake imeongeza masaa mawili katika shoo zake za Jumapili kwenye Ukumbi wa Garden Breez Magomeni, kutokana na maombi ya mashabiki wengi kutoka saa 6.00 hadi sa 8.00 usiku.

No comments:

Post a Comment