Monday, February 11, 2013

SERIKALI YAFUNGUA GHALA LA KISASA LA KUHIFADHIA DAWA KATIKA MAKAO MAKUU YA BOHARI YA DAWA (MSD), DAR ES SALAAM


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi  (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria upokeaji wa  magari  maalumu ya kusafirishia chanjo kwa  kuzingatia mnyororo badiri. Kushoto ni Mwakilishi  Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani  (UNICEF), DK. Jama Gulaid, Balozi wa Marekani  nchini Alfonso Lenhardt na Mbunge wa Temeke  Abbas Mtemvu. Mbali na kupokea magari hayo  kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mwinyi  alifungua Jengo la Kisasa la ghala la  kuhifadhi  dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya dawa  Dar es Salaam leo. (Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com)

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi  (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria upokeaji  wa magari  maalumu ya kusafirishia chanjo kwa  kuzingatia mnyororo badiri. Kutoka kushoto  ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Cosmas Mwaifwani,  Mwakilishi Mkazi wa Shirika  la kuhudumia watoto duniani (UNICEF),  DK. Jama Gulaid, Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt . Mbali na kupokea magari hayo  kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mwinyi  alifungua Jengo la Kisasa la ghala la kuhifadhi  dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya dawa  Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Cosmas Mwaifwani (kulia),akimuelekeza jambo  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein  Mwinyi (kushoto), juu ya ubora wa ghala  jipya la  kisasa la kuhifadhia dawa, baada ya kulizindua  katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD),  Dar es Salaam.  Wa pili kushoto ni Mbunge Viti maalunu Martha  Mlata na Balozi wa Marekani nchini   Alfonso Lenhardt.  
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein  Mwinyi,  akikata utepe kuashiria kupokea madawa na  vifaa tiba vilivyotolewa na Madaktari wa Afrika  kwa Serikali. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Tiba wa  Madaktari Afrika,  Dk.Dilan Ellegale na Balozi wa Marekani  nchini Alfonso Lenhardt.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi  (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya  pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya madawa  (waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu  Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, Balozi  wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu  Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa Kigamboni  Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la kuhudumia watoto duniani
(UNICEF),  DK. Jama Gulaid na Mbunge wa Temeke,  Abbas Mtemvu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein  Mwinyi (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa
katika picha ya pamoja na wawakilishi wa  Shirika la Afya Duniani ( (waliosimama nyuma).
Kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa  Serikali Donan Mmbando, Balozi wa Marekani
nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu Mkurugenzi   Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas
Mwaifwani,  Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine  Ndungululile,   Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
kuhudumia  watoto duniani (UNICEF),  DK. Jama Gulaid na  Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi  (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya  pamoja na wajumbe wa Kamati ya Afya ya Bunge  (waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu  Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando,  Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt,  Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa  (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa
Kigamboni  Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi  Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani  (UNICEF), DK. Jama Gulaid
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein  Mwinyi (hayupo pichani) akiwaongoza wageni
waalikwa wakati akipokea magari mawili maalumu ya kusafirishia dawa.
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa  (MSD), Cosmas Mwaifwani (kulia), akiwaongoza
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein  Mwinyi na Balozi wa Marekani nchini
Alfonso Lenhardt,  kwenda kuzindua magari maalumu ya  kusafirishia dawa.
Mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha  jinsi  ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa kutumia toroli maalumu.
Dereva wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha  jinsi  ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa
kutumia foku lifti.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein  Mwinyi (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali
kwenye hafla hiyo
Wafanyakazi wa Bohari ya Madawa (MSD), wakiwa
kwenye hafla hiyo
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Donan  Mmbando  akihutubia kwenye sherehe hiyo.


Na Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Afya na  Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi
 nchini kufanya msako na kuwafichua watu wote  watakaopatikana na dawa za Serikali
katika maduka binafsi.


 Maagizo hayo ylitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Rais Kikwete  ambaye angekuwa mgeni rasmi kwenye 
sherehe za  ufunguzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya
 Dawa jijini Dar es Salaam leo.


 "Natambua kuwa lipo tatizo la dawa na vifaa tiba vya serikali kupatikana katika maduka  ya dawa ya watu binafsi jambo ambalo linanikera sana nawaagizeni wachukukieni hatua  za kisheria wale wote watakao patikana na dawa hizo" alisema Rais Kikwete. Alisema Serikali haiwezi kuendelea kununua dawa  kwa dharama kubwa na zikaishia  katika mifuko ya watu wachache badala ya wananchi  walio wengi hususani wa vijijini. Alisema Bohari ya dawa iliundwa mwaka 1994,  ikiwa nadira ya kufikisha dawa na vifaa  tiba karibu na wananchi ambapo tumeambiwa  kuwa shughuli za MSD zimepanuka sana  hususani uwezo wa maghala umefikia mita za  mraba 51,800 na nusu ya hizo ni za  kukodisha kwa watu binafsi. 

"Natambua kuwa gharama za ukodishaji wa magahala ni kubwa sana na ni vema MSD
ikawa na maeneo yake yenyewe bila kutegemea  maghala binafsi" alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alizielekeza Halmashauri husika katika  kanda za MSD kuisaidia Bohari ya

dawa kupata maeneo mkakati ya uhifadhi wa dawa  na maeneo waliyonayo tayari

yaweze kupewa haki miliki. Alisema chanjo ni hatua muhimu kwa ajili ya ya afya 
za mama na mtoto ambapo mpango  wa taifa wa chanjo ulianza mwaka 1975 ukiwa unatoa 
chanjo dhidi ya magonjwa kama  Kifua Kikuu, Polia, Surua, Dondakoo, kifaduro na
 Pepo Punda. Alisema magonjwa mengine yaliyongezeka ni kinga 
dhidi ya Homa ya Ini, Homa ua Uti  wa mgongo, nimonia na kinga dhidi ya magonjwa 
ya kuhara. Rais Kikwete aliongeza kuwa kinga ni haki ya kila 
mtoto hivyo mahitaji ya chanajo  yamekuwa yanaongezeka kwaka hadi mwaka 
kutokana na ongezeko la idadi ya watu. "Ongezeko la idadi ya chanjo pamoja na ongezeko 
la aina za chanjo imesababisha kuwa  na hitaji kubwa la maeneo ya kuhifadhi chanjo na kuzisambaza" alisema Kikwete. Alisema Utunzaji wa chanjo unahitaji mfumo wa 
mnyororo baridi hivyo kuhitaji vyumba  maalumu vyenye ubaridi, pamoja na gari lenye 
vifaa vya kutunza ubaridi huo ili

kuhakikisha mnyororo baridi. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein 
Mwinyi alisema ufunguzi wa gahala hilo  ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa MSD wa 
kuhakikisha upatikanaji wa dawa

na vifaa tiba vyenye ubora unaokubalika na kwa bei nafuu. "Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Afya ya kufikisha huduma bora za  afya kwa kila Mtanzania" alisema Mwinyi.

Alisema vyumba vya kuhifadhia chanjo na magari  maalumu ya kusafirishia chanjo

uliozinduliwa vitasaidia katika kutunza na kusafirisha chanjo katika hali ya ubaridi kwa

mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ambayo Tanzania  inatekeleza.

Alisema ghala hilo linauwezo wa kuhifadhi  dawa na  vifaa tiba lina mita za mraba 4,280

na kuwa limejengwa kwa msaada wa Serikali ya  Marekani na Mfuko wa Dunia wa

Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na  limegharimu jumla ya Dola za Marekani

milioni 4 sawa na takribani sh.bilioni 6.4 za Kitanzania. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Cosmas Mwaifwani alisema ujenzi  wa ghala hilo ni matunda yaliyotokana na 
safari za  Rais Kikwete nje ya nchi hususan  Marekani ambapo mei 2 mwaka 2009 akiwa katika
 ziara nchini Marekani Rais wa nchi  hiyo Barack Obama aliahidi kuendelea kutoa 
misaada katika maeneo mbalimbali  likiwemo la kuboresha huduma za kupambana na 
maradhi ya Ukimwi kupitia shirika la  PEPFAR.

Alisema moja ya miradi inayoratibiwa na PEPFAR  ni ujenzi wa maghala makubwa katika

kanda za Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Tanga  na Tabora. Mwaifwani alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais  Kikwete kwani matokeo ya juhudi zake  zimeleta matunda ambayo yanaonekana kwa Taifa. Alisema ukamilishwaji wa miradi hiyo utaisaidia  Bohari ya Dawa kukomboa jumla ya

shilingi za Tanzania bilioni 1 katika mwaka  ujao wa  fedha ambazo wamekuwa wakilipa

kwa ajili ya kukodi maghala ya watu binafsi kwa ajili  ya kuhifadhi dawa, vifaa tiba na

vitendanishi kabla ya kusambazwa kwa walengwa. Alisema Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kusambaza  dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya hapa nchini 
kwa niaba ya Serikali. Aliongeza kuwa katika kutekeleza majukumu hayo 
Bohari ya Dawa imefanikiwa  kufanikisha upatikanaji wa dawa ambapo imefikia 
kati ya asilimia 70 hadi 75 ya mahitaji  dhidi ya asilimia 44 wakati Taasisi hiyo ilipo 
anzishwa mwaka 1994. 

Alisema mikoa 10 imeingizwa katika mfumo wa 
kufikisha dawa moja kwa moja hadi vituo vya afya na mikakati imewekwa ya kuingiza 
mikoa yote ya Tanzania katika mfumo  huo kuanzia julai 2013 na kuwa mkakati huu unazihusu pia hospitali za Wilaya, Mikoa na  Hospitali za Rufaa. Mwaifwani alisema MSD imefungua mfumo 
mpya wa kisasa wa TEHAMA (EPICOR) ili  kurahisisha shughuli za usambaji ambao pia umefadhiliwa na USAID.

No comments:

Post a Comment