Saturday, February 23, 2013

Skylight Band yatoa shukrani kwa mashabiki na kutambulisha nyimbo mpya ya 'Nasaka Dhoughs'




Mkurugenzi Mkuu wa Bendi ya Skylight Anneth Kushaba akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana ambapo ametoa shukurani kwa mashabiki na waandishi wa habari kwa kuiunga mkono bendi hiyo pamoja na kuwa bado ni changa. Ameongeza kuwa bendi hiyo inapiga muziki aina ya ‘Afro Pop’ kutokana na falsafa yao ya muziki na mahitaji ya soko la muziki wa ‘Live’ hapa Tanzania. Kulia ni mwanamuziki Joniko Flower.
Kushaba amewataka mashabiki wa muziki kuhudhuria kwa wingi katika show yao watakayopiga katika kiwanja chao cha nyumbani cha Thai Village kuanzia saa tatu usiku.
Mwanamuziki Joniko Flower wa Skylight Band akitoa kionjo kwa waandishi wa habari waliohudhuria hafla fupi ya kutambulisha nyimbo mpya na kuwashukuru mashabiki wao kwa kuwaunga mkono.
Aneth Kushaba AK 47 akiongoza kundi la vijana wa Skylight Band kutoa burudani wakati wakitambulisha nyimbo yao mpya ya "Nasaka Dhoughs" iliyomo kwenye albam yao yenye nyimbo nane inayokaribia kutoka hivi karibuni.
Sam Mapenzi akijimwaga na sebene la Carolina.
Mwanamuziki Sony Masamba akikamua.
Salma Yusuf uzao wa BSS akionyesha kipaji chake kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa single mpya ya Skylight Band.
Na Mo Blog.
Kwa niaba ya bendi nzima ya Skylight Mkurugenzi Mkuu Anneth Kushaba ameomba ushirikiano kutoka kwa mashabiki, hamasa na kuungwa mkono katika kuendeleza burudani na kuleta ladha mpya ndani ya fani ya Muziki.
Pia ameomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuendeleza juhudi za kuwahakikishia wapenzi wanaohudhuria maonyesho yao Thai Village kila Ijumaa wanapata muziki wenye kiwango bora kama unasikiliza CD.
Kushaba amesema wamefanikiwa kuboresha sauti kwa kuongeza aina ya vyombo vinavyotumika katika maonyesho ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment