MAKABIDHIANO: Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu
wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utoh (kushoto) akipokea mkataba wa
kumalizika kwa mradi wa awamu ya kwanza wa vituo 11 kutoka kwa Mkuu wa
Mauzo kutoka Kampuni ya SimuTanzania (TTCL), Bw. Tambwe Kisamba.
Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL na NAO wakimsikiliza Bw. Utoh
Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
DAR ES SALAAM,Tanzania
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imekabidhi vituo 11 vilivyounganishwa na
mkongo wa taifa kwa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali
uliogharimu shilingi milioni 477.
Akiongea katika halfa hiyo mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali Bw.
Ludovick Utoh ameishukuru TTCL kwa kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi
huo, na kuongeza kuwa uwepo wa mawasiliano hayo kutasaidia ofisi zote
za mkaguzi wa hesabu za serikali kuwa salama zaidi na kutaongeza
uadilifu kwani watakuwa na uwezo wa kuzuia tovuti ambazo hazina manufaa
katika utendaji wa kazi.
Aliongeza kuwa, faida nyingine ya mawasiliano hayo kutawawezesha kuanzisha mawasiliano ya ndani "intranet" hivi karibuni baada ya kupata mtandao wa uhakika kutoka TTCL, pia kupunguza kazi za makaratasi kwani sasa watakuwa wanatumia zaidi barua pepe kuwasiliana badala ya kuandikiana ujumbe mfupi kwa njia ya karatasi, kuwa na uwezo kwa kupokea taarifa kutoka mikoa mbalimbali kwa njia ya mtandao badala ya mtu kusafiri kutoka mkoani kuleta ripoti Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment