|
Mgeni
rasmi Profesa Elifas Bisanda wa Chuo Kikuu Huria akitoa nasaha zake za
kufunga mashindano ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki |
|
Zaidi ya makombe 80 yalikabidhiwa washindi |
|
Brass band ilikuwepo |
|
Wanamichezo wa
chuo kuikuu cha Kampala na baadhi ya lectures wao wakishangilia na
makombe yao waliyotwaa. Chuo hiki kilitwaa makombe 15. |
|
Mgeni
rasmi Profesa Elifas Bisanda wa Chuo Kikuu Huria akimkabidhi Profesa
Badru Kateregga wa chuo Kikuu cha Kampla kombe la mshindi wa kwanza wa
mpira wa miguu. |
|
Nahodha Okello
Maxwell wa timu ya chuo kikuu cha biashara cha Makerere (Makerere
University of Business School) akipokea kombe la mshindi wa pili kwa
soka baada ya kufungwa na Kampala kwa penalti |
|
Rais wa TOC Filbert Bayi akikabidhi kombe kwa timu ya kuogolea |
|
|
|
Wakati Vyuo vya Uganda na Kenya vikiondoka na medali na makombe kibao
vyuo vikuu vya Tanzania imeambulia mikono mitupu kwani ni Chuo Kikuu cha
Mlima pekee kilichopata kombe kwa mchezo wa chess tena kwa nafasi ya
tatu.
Tanzania ambayo ilikuwa wenyeji imetiaaibukwani pamoja na kuwa na vyuo
vikuu vingi ni vyuo vikuu saba yt viliyoleta wawakilishi huku Kenya na
Uganda wakileta vyuo 17 kila mmoja.
Zaizi ya makombe 80 yamekabidhiwa kwa washindi huku Chuo Kikuu cha Kampala na Ngejje wakitia fora kwa kuondoka na makombe mengi
Chuo Kikuu cha Kampala ambacho ndio mabingwa kwa mchezo wa soka
kimechukuwa makombe 15 na mwakani mashindano ya vyuo Vikuu vya Afrika
mashariki yatafanyika nchini Uganda.
Mshindi wa pili kwenye soka ni chuo kikuu cha biashara cha Makerere
baada kufungwa na Chuo kikuu cha Kampala wenzao toka Uganda kwa penalti
4-5 baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa hawajafungana ndipo zilipopigwa
penalti ili apatikane mshindi.
Vyuo vikuu vyauganda vimefanya vizuri kwani ukiangalia kwenye
miichezo kikapu, wavu, soka, handball wanawake na wanaume wameingia
fainali wenyewe.
No comments:
Post a Comment