Monday, February 11, 2013

WAZIRI MEMBE AKAGUA UJENZI KIWANDA CHA SARUJI LINDI.


Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe (wapili kushotoakikagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda Cha Cement Mkoani Lindi leo, ambako Kiwanda hicho kinajengwa na kutarajiwa kutoa ajira kwa zaidi ya watu 600.
Akipewa maelekezo na wasimamizi wa mradi huo na kampuni inayojenga.
Akiangalia vifaa vitakavyotumika kwenye ujenzi.
Vifusi vikiendeleo kushushwa kwenye eneo hilo.
Vitendea kazi vya kutosha kwenye eneo hilo vinaonekana huku kukiwa na vijana zaidi ya 250 wakiwa wamepata ajira za muda.
Baadhi ya vitendea kazi kwenye eneo hilo.
Na Abdulaziz video,Lindi
Zaidi ya Wakazi 600 wa Manispaa ya Lindi watanufaika na Ajira mara
utakapokamilika Ujenzi wa Kiwanda cha Simenti kilichoanza hatua za
awali za Ujenzi wake huku Tayari zaidi watu 250 wakiwa wamepata ajira
katika hatua za awali baada ya kuanza kwa kazi hiyo hivi karibuni
Akizungumza na Wakazi wa Manispaa ya Lindi mara baada ya kukagua kazi
za Ujenzi wa kiwanda hicho kilichoanza ujenzi kufuatia Upatikanaji wa
Gesi katika Mikoa ya Lindi na Mtwara,Waziri wa mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe alitoa wito kwa Wazazi na
walezi kuongeza jitihada za kusomesha watoto ili wanufaike na ajira
zitakazopatikana kutokana Uwepo wa Viwanda na shughuli mbalimbali
zinazotokana na Gesi ikiwemo Upanuzi wa Bandari ya Lindi ya Mji wa
Lindi
Waziri Membe alitembelea kukagua kazi za ujenzi wa Kiwanda hicho
Maeneo ya Machole Manispaa ya Lindi ambapo alielezwa kazi
inavyoendelea na ajira zilizopo kwa  sasa
Sambamba na Gesi ya Mtwara,Waziri Membe alibainisha kuwa Kampuni ya
Satoil ya Norway tayari imegundua uwepo wa Gesi nyingi umbali wa Km 85
baharini kutoka manispaa ya Lindi na kupatikana kwa gesi hiyo,Serikali
tayari Imeshaingia mikataba ya Uchimbaji wake
‘’’’Gesi hiyo iliyogunduliwa na kampuni ya Satoil itasaidia maendeleo
ya Lindi kwa kuwa kutajengwa kiwanda cha Mbolea,Kiwanda cha vifaa vya
plastiki aina zote pamoja na Upatikani wa uhakika wa nishati ya Umeme
alimalizia Membe kwa kusema Lindi Kucheleeeee!!!!!”””
Awali akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake,Meneja Mradi wa
Lindi Cement kiwanda ambacho kinajengwa na Kampuni ya Meis
Industries,Bw Valerian Magembe alibainisha kuwa kazi ya Ujenzi wa
kiwanda hicho itakamilika na kuanza Uzalishaji June 2014 ambapo zaidi
ya wananchi 600 watanufaika na Ajira na kueleza kuwa kiwanda hicho
kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 500 kwa siku
Ndg Waandishi mipango yetu iko vema kama mnavyoona kazi inavyoendelea
na tayari Maji na Umeme ndio tunakamilisha,,Wana Lindi wakae mkao wa
kula kwa kupata ajira na ongezeko la pato la kila mdau kwa sekta
yake…Na pia nawahakikishia kiwanda hiki ni cha kisasa na hakutokuwa na
uharibifu wa Mazingira kutakuwa na mtambo wa kudhibiti
Vumbi..Tumejipanga vilivyo…Alimalizia Bw Magembe
Kazi za Ujenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Kampuni ya Wazawa
ya  Meis Industries kinatarajiwa kuzalisha tani 500 kwa siku
kitakapokamilika huku tayari ajira zaidi ya 250 zimetolewa kwa wakazi
wa mji huo kwa awamu ya kwanza ya kazi za Ujenzi

No comments:

Post a Comment