Tuesday, February 26, 2013

WAZIRI WA MAMBO YA NNJE WA OMAN AKUTANA NA DK.SHEIN.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo,
Balozi wa Tanzania Nchini Oman,Ali Ahmed Saleh, (kushoto) Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati  wa nchi za Nje,Hassan Simba Yahya (kati) na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Said Shaib Mussa, walipoungana na katika mazungumzo ya Ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman, ukiongozwa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah, (hayupo pichani ) na Rais wa Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo, kwa ajili ya Mazungumzo na Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza  na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,ukiongozwa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin
Alawi Bin Abdullah,(wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo,kwa ajili ya Mazungumzo na Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,ukiongozwa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah,(wa pili kushoto) baada ya mazungumzo yao  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar, Picha na Ramadhan Othman,IKulu.

No comments:

Post a Comment